Featured

    Featured Posts

WANANCHI WASHIRIKI UJENZI WA HOSPTALI YA WILAYA YA KIGOMA INAYOJNGEWA NA SERIKALI KATIKA KATA YA MAHEMBE KWA ZAIDI YA SH. BILIONI MOJA

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Simon Chacha akishiriki kuchimba Msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inayojengwa kwenye Kata ya Mahembe.

Mwandishi Maalum, Kigoma
Serikali imeanza Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ili kukabiliana na changamoto ya wananchi wa Wilaya hiyo ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya na ujenzi utagharimu sh. Bilioni moja na milioni mia tano hadi kukamilika kwake.

Katika kuhakikisha matokeo chanya, Wananchi wa Kata ya Mahembe inapojengwa Hospitali hiyo, wamejitokeza kuchangia nguvu zao katika shughuli ya Uchimbaji wa Msingi  wa Jengo ambalo baada ya kukamilika kwake litawaondolea adha ya kutembea takribani Kilometa nane kufuata huduma za Afya.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa ujenzi wa Msingi wa Hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk. Simon Chacha amesema ujenzi wa Hospitali hiyo umepangwa kukamilika  mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti,  baadhi ya wakazi wa Mahembe wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea maendeleo hatua ambayo haikuwahi kufikiwa kwa miaka mingi iliyopita. 

"Muda tuliokuwa tukiutumia kwenda umbali mrefu kutafuta tiba au kupeleka huduma mbali, tutautumia kuendeleza shughuli zetu za kiuchumi" walisema. 

Aidha, wameipongeza Serikali kwa kufikia Uchumi wa kati kabla ya muda uliopangwa huku wakionesha matumaini makubwa ya maendeleo ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Pendo Mangalia amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma katika maeneo ya karibu na kuwaondoa na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma.

Amesema wananchi wamehamasika na kuchangia nguvu zao kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Kukamilika kwa  ujenzi wa hospitalii hiyo katika eneo la Mahembe kunafanya kuwa na Hospitali Tano za Wilaya Mkoani Kigoma.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana