Featured

    Featured Posts

PSSSF SASA KIDIJITALI, YAANZISHA HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere (kulia), akisaidiwa kuangalia michango yake katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Kaimu Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Abdul Njaidi (wapili kushoto) na Afisa Matekeleza Mwandamizi wa Mfuko huo, Donald Meeda wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, lililopo katika Viwanja vya Julius Nyerere maarusu Viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, leo, Julai 5, 2020.

Na Maalum, Sabasaba
Ikiwa ni miaka miwili tu tangu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) uanzishwe, sasa Mfuko huo umekuja na mfumo wa kisasa wa kutoa huduma kwa wanachama wake kupitia njia ya mtandao (online portal) ili kurahisisha zaidi huduma zake.

Akizungumzia mfumo huo wa Kidijitali, Mhandisi wa Mifumo ya Kompyuta (System Engineer) wa Mfuko huo Injinia Goodluck Msangi amesema, mfumo huo ambao pia kufanya kazi kwenye banda la PSSSF lilipo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba,amesema unawawezesha wanachama na wastaafu kupata taarifa mbalimbali kuhusu mwenendo wa michango na taarifa za malipo ya pensheni ya kila mwezi.

“Kwa wanachama wanaweza kupata taarifa ya mwenendo wa michango yao iliyowasilishwa na mwajiri na mstaafu ataweza kupata taariza za malipo ya pesnheni ya mwezi kiasi kilicholipwa na Benki ambayo kiasi hicho cha fedha kimelipwa na pia  mfumo huo unawezesha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwanachama au mstaafu na PSSSF wakati wowote na mahala popote bila ya mhusika kulazimika kufika kwenye ofisi za Mfuko.” Alifafanua Enjinia Msangi.

Amesema, kupitia mfumo huo wa kidijitali, endapo mwanachama ana maoni, ushauri au anahitaji ufafanuzi wa jambo lolote anaweza kufanya hivyo na mrejesho akaupata mara moja na kwamba mfumo huo unapatikana kwenye tovuti ya mfumo kwa kubofya www.psssf.go.tz
Habari zaidi katika Picha, Tafadhali../BOFYA HAPA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana