RAIS DK. MAGUFULI
Ikulu, Chamwino.Rais Dk. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Julai, 2020 amemteua Albinus Mgonya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro huku akimteua Waziri Khachi Kombo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.
Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Gerson Msigwa, imesema, kabla ya uteuzi huo, Mgonya alikuwa Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Rukwa na anachukua nafasi ya Mohamed Musa Utaly.
Imeongeza taarifa hiyo kwamba, kabla ya uteuzi Kombo yeye alikuwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro na amechukua nafasi ya Wendi Ng’ahala na kwamba uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 05 Julai, 2020 na wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma, kesho tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.
Post a Comment