Rais Dk. John Magufuli amemteua Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mariam Perla Mmbaga kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Taarifa ya Ikulu imesema.
Taarifa hiyo imesema Mariam Perla Mmbaga anachukua nafasi ya Jumanne Sagini na ataapishwa Jumatatu tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.
Post a Comment