Featured

    Featured Posts

WANACHAMA WA PSSSF WAHIMIZWA KUFIKA KWENYE OFISI ZA MFUKO HUO KOKOTE HAPA NCHINI KUHAKIKI TAARIFA ZAO

Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe (kulia), akimuhudumia Mwanachama aliyefika kwenye banda namba 13 la Mfuko huo wa PSSF lililopo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana, Julai 3, 2020. 

Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.
WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamehimizwa kufika kwenye ofisi za Mfuko huo zilizoenea katika mikoa yote nchini ili kuhakiki taarifa zao kwa ajili ya kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadaye taarifa hizo zitakapohitajika.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, katika banda namba 13 la Mfuko huo kwenye Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana, Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe amesema mwanachama akifika kwenye ofisi yoyote ya PSSSF atapatiwa huduma hiyo bila usumbufu.

Meneje huyo amesisitiza na kuhimiza kila mwanachama wa PSPF kufanya hivyo kwa kuwa ni muhimu sana ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadaye ikiwemo kupoteza muda mwingi taarifa zitakapokuwa zinahitajika.

Pia amewaalika wanachama watakaofika kwenye Maonyesho hayo maarufu kama Sabasaba, katika Viwanja vya Julius Nyerere kwenye, wafike kwenye banda la PSPF kujipatia huduma zote kama zinavyotolewa kwenye ofisi za Mfuko kwenye mikoa yote nchini.

“Tulichofanya mwaka huu tumehamisha miundombinu na vifaa vyote vya kutoa huduma vinavyopatikana kwenye ofisi zetu ikiwemo makao makuu, hivyo mwanachama anapofika kwenye banda letu anapata huduma zote ikiwemo, taarifa za michango, mafao, pensheni na mafao yanayotolewa na Mfuko" alifafanua Mlowe. 

Maonesho hayo yaliyoanza Julai 1, 2020 yamefunguliwa rasmi jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa viwanda, ajira na biashara endelevu”.
Meneja wa Mfuko wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe, akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Abdul Njaidi (kulia) na Afisa Uhusiano pia wa Mfuko huo, Meseka Kadala kwenye Banda namba 13 la Mfuko huo wa PSSF lililopo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, jana, Julai 3, 2020. PICHA ZAIDI...BOFYA HAPA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana