Featured

    Featured Posts

WANAHABARI WAFURAHISHWA NA MAFUNZO YA JINSI YA KURIPOTI HABARI ZA MKUTANO MKUU WA CCM

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG).  Ernest Sungura akifafanua jambo jinsi ya kuandika habari kwa ufasaha kwa kuzingatia Katiba ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM), wakati  wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho unaofanyika kwa siku mbili  Julai 11 -12, 2020 jijini Dodoma. 

UMG inamiliki magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Kituo cha Radio cha Uhuru FM.
.
Mafunzo hayo yaliyowashirikisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari watakaoripoti mkutano huo yamefanyika katika Ofisi za Uhuru, Dodoma, kwa uratibu wa Chama cha  Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na UMG. 

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waripoti kwa usahihi matukio muhimu ya mkutano huo. Wakufunzi wengine waliotoa maada ni; Mwanzo Millinga Mhariri wa Mitandao ya Kijamii (UMG), Josephat Mwanzi, Msaidizi wa CEO Kimkakati (UMG).


 Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mafunzo hayo
 Jasmane Shamwepo Mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Mwangaza FM, akieleza jinsi alivyofurahishwa na mafunzo hayo yaliyomwezesha kupata uelewa kuhusu Katiba ya CCM  na utaratibu  wa mkutano mkuu.
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira, akielezea jinsi mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza kwa wanahabari, jinsi yalivyomfumbua kwa kujua mambo mengi kuhusu Katiba ya chama hicho, hivyo kumsaidia kuandika kwa ufasaha habari za mkutano huo.
 Anastazia Anyimike wa Habari Leo
 Sakina Masoud wa Uhuru FM, Inayomilikiwa na CCM
 Agusta Njoji
 Mwanahabari Saida Issa wa Gazeti la Zanzibar Leo
 Oliver Nyeriga EATV na EARADIO
 Joyce Mwakalinga wa TBC
 Happy Mtweve wa Gazeti la Uhuru
 Mpiga Picha wa Gazeti la Daily News, Iddy Mwema
 Fred Alfred wa Gazeti la Uhuru
 Josephine Kaponya wa EFM na TVE
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa UMG, Sungura akihitimisha mafunzo hayo na kuahidi maoni mbalimbali yaliyotolewa na wanahabari katika mafunzo hayo, kuyawasilisha kwa uongozi wa CCM ili yafanyiwe kazi kwa lengo kwamba siku za usoni kuwepo na utaratibu mzuri wa kuendesha mafunzo ya namna hiyo.
 Aboubakar Famau wa BBC
 Mwanahabari mkongwe wa Gazeti la Uhuru, Bakari Mkondo, aliwataka wanahabari kuacha tabia ya kuandika habari kwa chuki bali waandike kwa kufuata maadili ya uandishi bila upendeleo
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana