Featured

    Featured Posts

WAZIRI ZUNGU ATEMBELEA BANDA LA MOI KATIKA MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA VIWANJA VYA SABASABA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano na Mazingira) Mh. Mussa Azzan Zungu akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Patrick Mvungi (mkuu wa kitengo cha uhusiano MOI) kuhusu namna MOI inavyotoa huduma za kibingwa za mifupa kwa watanzania. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Dkt Angel Lameck akimhudumia mgonjwa alipofika katika banda la MOI kupata huduma.
 Mjumbe wa bodi ya wadhamini MOI, Dkt Petronila Ngiloi akisikiliza maelezo kutoka kwa wataalam wa MOI kuhusu huduma mbalimbali alipotembelea banda la MOI katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa Julai 7, 2020 Dar es Salaam.
 Dkt Sharif Luena akitoa elimu kuhusu mfumo wa uti wa mgongo kwa washiriki wa maonyesho ya sabasaba waliotembelea banda la MOI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano na Mazingira) Mh. Mussa Azzan Zungu akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Geofrey Mwakasungura (Mkuu wa kitengo cha karakana ya viungo bandia MOI) kuhusu matibabu ya magoti kwa njia ya matundu (Knee Athroscopy) alipotembelea banda la MOI leo.

NA KHAMISI MUSSA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano na Mazingira) Mh. Mussa Azzan Zungu akisikiliza maelezo kutoka kwa(Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu ametembelea banda la Taasisi ya tiba ya mifupa MOI na kupongeza huduma bora 
zinazotolewa na MOI. 

Akiwa katika banda la MOI Mh Zungu amepata maelezo ya kina ya namna taasisi ya MOI inavyotoa huduma zake za kibingwa kwa wananchi jambo ambalo limepelekea kumaliza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.

Akitoa maelezo ya namna huduma za MOI zilivyobotreshwa mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MOI Bw. Patrick Mvungi amesema huduma za MOI zimeimarika sana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya Tano ambapo kwa sasa vifaa vyote vya uchunguzi vinapatikana MOI.

Bw. Mvungi pia amemueleza Mh Zungu kwamba taasisi ya MOI inatumia teknolojia ya hali ya juu katika kutoa huduma za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu akitolea mfano aina ya antena ambayo inatumika kumsaidia mgonjwa kufidia kipande cha mfupa kilichopotea.

Taasisi ya MOI inashiriki katika maonyesho ya 44 ya sabasaba ambapo washiriki wanapata huduma , ushauri pamoja na elimu kuhusu huduma za MOI pamoja na magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana