Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasan akijadili jambo na Wajumbe wenzake wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Spika wa Bunge Job Ndugai na Spika wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulidi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akijadili jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipitia makabrasha wakati wa kikao hicho ambacho pamoja na mambo kilikuwa cha kupitia majina ya walioomba kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya CCM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt Ali Mohamed Shein wakitoka nje ya ukumbi kwa mapumziko mafupi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM leo Jumanne Agosti 18, 2020 jijini Dodoma
Post a Comment