Featured

    Featured Posts

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA BoT, NANENANE SIMIYU

NA KHALFAN SAID, NYAKABINDI
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu ikiwa ni miongoni mwa shughuli alizofanya wakati akifungua rasmi Maonesho ya mwaka huu ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja hivyo.

Makamu wa Rais alipokewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dk. Bernard Kibesse na Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Zalia Mbeo na kutembelea idara mbalimbali za Benki hiyo na kuelezwa jinsi zinavyowahudumia wananchi wanaofika kwenye banda hilo.

Maonesho ya mwaka huu ambayo yamebeba kauli mbiu ya “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020."

Lengo hasa la Maonesho hayo yanayofanyika kitaifa kwa mara ya tatu mfululizo kwenye viwanja hivyo ni kutoa fursa kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika kuona na kujifunza matumizi ya teknolojia Bora za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija na uhakika wa chakula, kukidhi mahitaji ya viwanda na masoko.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT, Vicky Msina (katikati) huku Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibesse (kulia) akishuhudia wakati Kiongozi huyo alipotembelea banda la Benki Kuu kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo nya mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambako maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu wa 2020 yanafanyika. Makamu wa Rais alifungua rasmi maonesho hayo, leo.
 Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Zalia Mbeo (kushoto) akimuongoza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kutembelea banda hilo.
 MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfuko wenye machapisho mbalimbali yanayoelezea shughuli za BoT kutoka kwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Bernard Kibesse wakati alipotembelea banda hilo leo Agosti 1, 2020
Makamu wa Rais akiondoka wkenye banda la BoT baada ya kulitembelea.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana