MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanza rasmi kulipa Fao la Uzazi kwa wanachama wake wanawake.
Akizungumza kwenye banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya Nanenane yaliyokuwa yakifanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba alisema malipo hayo yameanza ikiwa ni takriban miaka miwili tangu Serikali iunganishe Mifuko minne ya hifadhi ya jamii ya PSPF, PPF, LAPF NA LAPF na kuundwa PSSSF.
“Nanenane ya mwaka huu ni tofauti kidogo kwetu maana tumekuja na fao la uzazi, fao ambalo lilikuwa halijaanza kutolewa baada ya mifuko kuunganishwa mwezi huu wa nane (8) tumeanza kulipa fao la uzazi kwa wanachama wetu wanaojifungua wakiwa kazini.”
Akitaja vigezo vinavyozingatiwa kulipa fao hilo, Bw. Kashimba alibainisha kuwa ni lazima mnufaika awe ni mwanachama wa PSSSF mwanamke aliyechangia kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu (3) na anapaswa kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika kwenye mfuko ndani ya siku Tisini (90) baada ya kujifungua.
Akifafanua zaidi kuhusu masharti hayo alisema, “Fao hilo la uzazi mwanachama anaweza kufaidika nalo kwa uzao wa kwanza, wapili, watatu hadi wanne haijalishi katika moja ya uzao huo kajifungua mtoto mmoja au mapacha au kila uzao kajifungua mapacha, kinachozingatiwa hapa kwa mmujibu wa sheria ni kwamba mwachama atafaidika na fao hilo mara mara nne.” Alisema Bw. Kashimba.
Alisema maonesho hayo ya mwaka huu ambayo yamefikia kilele leo Agosti 10, 2020 baada ya Waziri wa Kilimo Bw. Japhet Hasunga kuongeza siku mbili zaidi za maonesho kutoka Agosti 8 ambayo ni kilelel cha siku ya Wakulima hadi Agosti 10, ili kutoa fursa zaidi kwa wanachi kufaidika na maonesho.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba (aliyekaa kushoto), akimsikilzia mwanachama wa mfuko aliyetembelea banda la PSSSF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. Maonesho hayo yaliyofikia kilele Agosti 8, 2020 yaliongezwa siku mbili zaidi hadi Agosti 10, ili kuwapa fursa wananchi kuhudumiwa.Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko was Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (wakwanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga wakiangalia michango yao kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) huhu wakipata usaidizi kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bi. Rehema Mkamba, kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Post a Comment