Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKUU LEBANON AJIUZULU

 

  Waziri  mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza kujiuzulu kufuatia mripuko wa wiki iliyopita mjini Beirut.

Kwenye taarifa yake fupi kupitia televisheni, waziri mkuu Diab alisema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko. 

Rais Michel Aoun amekubaliana na hatua hiyo ya serikali kujiuzulu. 

Wiki iliyopita Diab alimlaumu mtangulizi wake kwa mripuko huo. 

Alisema wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndio umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali kuibuka baada ya mripuko huo kutokea.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana