Na: Faustine Gimu
Waziri wa Mambo yaNdani George Simbachawene amevitaka vyombo vya usalama nchini kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Usafirishaji wa binadamu ambayo imekuwa ikifanyika ndani ya nchi na nje ya nchi.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu yaliyohusisha wadau mbalimbali ambapo biashara hiyo hufanyika mataifa mbalimbali duniani.
Amebainisha kuwa Wizara itajikita kusimamia safari za ndani ya nchi kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo ambapo amebainisha kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na watoto vitendo ambavyop hutokana sababu mbalimbali ikiwemo tama ya pesa na kuibuka kwa soko la vitendovya ngono.
Akizungumzia watanzania wanaotaka kufanya kazi nje ya nchi amewata kufuata sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kuzamia kwa kutumia njia haramu kwa kigezo cha kutafuta maisha akisisitiza kujiridhisha kuhusu kazi husika kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kuzuia na Kupamba na biashara haramu ya usafirishaji wabinadamu Amatus Magere katika amesema mapambano hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi kwani hufanywa na binadamu wenyewe kwa siri kubwa ,kukosekana kwa mfuko wa kusaidia waathirika na upungufu wa raslimali watu
Post a Comment