Na Mwandishi wetu, Simiyu
WAAJIRI waliofika kwenye banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, wamefurahishwa na elimu waliyopata kuhusu namna ya kutoa taarifa za mfanyakazi aliyepata ajali na magonjwa yatokanayo na kazi au kifo kupitia njia ya mtandao (Online Notification System).
“Shughuli kubwa iliyonileta hapa kwenye banda la WCF ni kupata maelekezo na elimu kuhusu namna ya kutumia mtandao kujisajili na kuwaorodhesha wafanyakazi wangu katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) lakini pia jinsi ya kutoa taarifa endapo mfanyakazi atapata ajali kutokana na kazi ili aweze kulipwa fidia.”
Kaimu Meneja Mkuu wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ednand Magenda, amesema elimu aliyopata kutoka katika banda la WCF imemsaidia sana na kwamba ataitumia mara moja kwanza kujisajili na kuwaorodhesha wafanyakazi wake ili na wao waweze kuhudumiwa na Mfuko pindi watakapopatwa na majanga wawapo wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi.
“Nimeelekezwa jinsi ya kuwaorodhesha na nitaanza kuwasilisha michango yao mara moja kwenye mfuko kupitia mtandao kama nilivyoelekezwa.” Alisisitiza Bw. Magenda.
Naye Meneja wa kampuni ya Dag Farm Company Limited iliyoko Wilayani Tarime mkoani Mara Bw. Nicholous Babere alisema amefurahishwa na huduma aliyoipata kwenye banda hilo kwani imemuwezesha kuelewa namna ya kujisajili na kutoa taarifa ya mfanyakazi aliyeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi kupitia mtandao.
“Tulipata taarifa hii siku za nyuma lakini nilikuwa bado kujisajili, nimefika hapa kwenye banda la WCF, nimepata elimu ya kutosha na nimefurahia na kuahidi kwamba mwezi huu kampuni itajisajili ili wafanyakazi wetu nao waweze kupata huduma kutoka taasisi hii ya serikali ya WCF inayowahudumia waajiri wote na waajiriwa walioko katika sekta binafsi na umme.” Alisema Bw. Babere.
Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ednand Magenda (mwenye kofia) na waajiri wengine, wakielimishwa jinsi ya kuwasilisha taarifa za mfanyakazi aliyepata ajali, kuugua au kifo kutokana na kazi kupitia njia ya mtandao yaani Online Notification System kutoka kwa Afisa katika ofisi ya Utawala, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Neema Mushi katika banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu Agosti 6, 2020.
Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ednand Magenda (mwenye kofia) na waajiri wengine, wakielimishwa jinsi ya kuwasilisha taarifa za mfanyakazi aliyepata ajali, kuugua au kifo kutokana na kazi kupitia njia ya mtandao yaani Online Notification System kutoka kwa Afisa katika ofisi ya Utawala, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Neema Mushi katika banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu Agosti 6, 2020.
Afisa katika ofisi ya Utawala, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Neema Mushi (kushoto), akitoa elimu kuhusu masuala ya fidia kwa wananchi waliofika kwenye banda la WCF viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.Afisa Uhusiano Mwnadamizi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), akimkabidhi zawadi Menja wa kampuni ya Dag Farm Company Limited iliyoko Wilayani Tarime mkoani Mara Bw. Nicholous Babere alipotembeela banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Agosti 6, 2020.
Post a Comment