Naibu Mkurugenzi wa Uhuru FM Abdalah Huseni akimhoji Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kwa tiketi ya CCM Dk. Alfred Kimea wakati kikosi kazi cha Amsha Amsha ya Uhuru FM kilipokuwa Mjini Korogwe leo.
Na Pius Ntiga, Korogwe
Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Korogwe Mjini Mkoani Tanga kimesema mageuzi makubwa na ya haraka yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, yanakipa ushindi wa kishindo chama hicho Oktoba 28 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa Leo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Korogwe Mjini Emanuel Chale katika mahojiano na kikosi kazi cha Amsha Amsha Cha Uhuru FM Mjni Korogwe.
Katika Mahojiano hayo Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya amesema miradi ya kimkakati kama Elimu, Afya, Miundombinu, Kilimo kupitia umwagiliaji inaiba ushindi CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Ujao.
Tayari amesema serikali katika Wilaya ya Korogwe Mjini imetoa kiashi Cha shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya mradi wa Maji wa kwa Msisi ambao unetatua kero iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Korogwe kwa muda mrefu ambapo Sasa haipo Tena.
Aidha, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ilielekeza kuwa Huduma ya maji maeneo ya mjini iwe asilimia 90 na vijijini iwe asilimia 80, ambapo kwa ujumla hadi Sasa utekelezaji wa Maji unefikiwa kwa asilimia 85 nchi nzima.
Kwa upande wake mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini Dkt Alfred Kimea ambaye ni mtaalamu wa Biashara na Kodi amesema akishinda atahakikisha anawaunganisha wananchi hasa vijana kupitia mitaji ya kibiashara na kwa wasajiriamali pia.
Aidha, amesema kupitia Ilani ya CCM inayonadiwa ya mwaka 2020-2025 inayoielekeza serikali ijayo kutengeneza ajira Milioni nane, mgombea huyo Ubunge amesema atatumia Elimu yake ili kufikiwa kwa idadi hiyo ya ajira kwa vijana wakiwemo wa Korogwe.
Kuhusu Ununuzi wa Ndege 11 zilizonunuliwa na serikali, amewataka wananchi kuwapuuza wapinzani kwani amesema faida ya Ndege hizo inaonekana kupitia fedha zinazopatikana kwa kubeba watalii, wafanyabiashara na wananchi kunufaika zaidi .
Naye Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Korogwe Mjini Omar Sempole amesema kama vijana wamejipanga ipasavyo kulinda kura za CCM walitekeleza agizo la Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ali alilowataka vijana mwaka huu kulinda kura hizo.
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kuwa watulivu kwa kuwa chama kimesema mwaka huu kampeni zake zitakuwa ni za kistaarabu.
Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CCM alizipa maagizo JUMUIYA za chama hicho kulinda na kuzitafuta Kura za chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kikosi Kasi Cha AMSHA Amsha Cha Uhuru FM kipo katika kampeni yake ya kupitia maeneo ya kimkakati yaliyoainishwa na kutekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.
Pia kikosi kazi hicho kitaifikia Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo leo kilikuwa Korogwe Mkoani Tanga.
Post a Comment