Featured

    Featured Posts

KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI ERASTO SIMA APIGA 'SHOTO-KULIA' MITAANI KUSAKA KURA ZA RAIS, MBUNGE NA MADIWANI KATIKA KATA YA MSOGOLA, DAR ES SALAAM, LEO


Na Elisa Shunda, Dar Es Salaam.
RAI imetolewa kwa wakazi wa jimbo la Ukonga kutorudia kuionja sumu kwa ulimi kwa kuchanganya wawakilishi katika nafasi ya ubunge na udiwani katika uchaguzi wa mwaka huu uliopangwa kufanyika Oktoba 28.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwalimu,Erasto Sima, wakati akizungumza na wakazi wa eneo la Mvuti kwenye Ufunguzi wa Kampeni za chama hicho katika Viwanja vya CCM Kata ya Msongola, wilayani Ilala, jana.

Aidha Katibu Mkuu Huyo wa jumuiya ya Wazazi, Sima, alisema katika uchaguzi wa mwaka 2015 wakazi wa jimbo la Ukonga waliamua kuionja sumu wenyewe bila kushurutishwa na mtu kwa kumchagua Rais.Dk.John Magufuli, Mbunge Atokanaye na Upinzani na Diwani wa CCM Hali iliyozorotesha maendeleo.

"Ndugu zangu wakazi wa jimbo la Ukonga sumu haionjwi kwa ulimi, uchaguzi uliopita hapa mlikosea wamakonde wanaita mlitindinganya mambo kwa kumteua Rais, Dk.Magufuli, Mbunge wa Upinzani ingawa baadae aliludi ccm ikawa muda umepita wa Kutekeleza kero za wananchi na diwani wa ccm;

"Sisi wanachama wa CCM tunaamini maendeleo ya kweli yanapatikana kwa mafiga matatu yaan Rais wa CCM,Mbunge wa CCM na Diwani wa CCM, hata mmoja wao akikosea anaitwa na chama anaonywa kazi inaendelea, hivyo nawaomba msituchanganyie machungwa na malimao kwenye kapu moja hatuendi hivyo" Alisema Sima.

Pia katika Uhamasishaji wa wakazi wa jimbo la Ukonga kujitokeza kuwapigia kura za ndio wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais.Dk.Magufuli, Mbunge Jerry Silaa na Madiwani wote wa chama hicho, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Sima, alitembelea nyumba kwa nyumba, madukani, magengeni na mtu kwa mtu katika sehemu mbalimbali kuomba kura za ndio kwa CCM.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar Es Salaam, Frank Kamugisha, akimkaribisha Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kuzindua kampeni za kata ya Msongola, amemhakikishia awamu hii kwa utekelezaji na uchapakazi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Mgombea wa CCM Nafasi ya Urais, Ndugu Dk.John Magufuli kwa sauti moja wananchi wa jimbo la Ukonga wataipigia kura ya ndiyo CCM.

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia tiketi ya CCM, Jerry Silaa, alisema wakati akiwa Meya wa manispaa ya Ilala alipigania kituo cha afya ambacho fedha zake zilitoka kwa wafadhili kinajengwa kata ya Msongola lengo kusogeza huduma hiyo kwa wananchi, hivyo amewasihi wamchague akawasemee bungeni sehemu ya barabara iliyobakia ijengwe na kutatua changamoto zingine.

Hata hivyo Mgombea Udiwani wa Kata ya Msongola, Aziz Mwalile, akizungumza katika ufunguzi wa kampeni hiyo alisema kwamba mara kwa mara alikuwa akipambana kutetea kata hiyo kwa machache kufanikiwa na mengineyo kushindikana kutokana na muunganiko wao kuwa mbovu kwa jini kisirani kuwepo katikati yao, hivyo amewasihi wananchi wa jimbo la Ukonga na kata ya Msongola kutofanya makosa wachague mafiga matatu.

Akisalimia katika mkutano huo, mjumbe kamati ya Utekelezaji jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar Es Salaam, Mohamed Sangaraza, alisema kwamba ukienda dukani ukanunua tochi na betri mbili katikati ukaweka gunzi taa ya tochi haitowaka ng'oo .

hivyo Mjumbe, Sangaraza aliwaomba wakazi wa jimbo la Ukonga kwa kusema uchaguzi uliopita walikosea kwa kununua betri mbili na kuweka kwenye tochi badala ya betri tatu, amewaomba mwaka huu kutofanya makosa ifikapo oktoba 28 mwaka huu ni mwendo wa mafiga matatu yaani Kupiga kura za ndiyo kwa rais,mbunge na madiwani wote watokanao na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana