Featured

    Featured Posts

CCM KUSIMAMIA MAKUSANYO YA MAPATO YA NDANI

 Na Scolastica Msewa, Kisarawe.

Serikali ya Chama cha Mapinduzi itaendelea kusimamia ukusanyaji mapato ya ndani ambayo asilimia 10 hutolewa kikopo kwa Vijana Wanawake na wanaoishi na Ulemavu.


Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Matitu Vulu wakati akiomba kura za kishindo kwa Wagombea wa CCM katika mkutano wa kampeni katika kata ya Msanga kijiji cha Bembeza na Msanga sokoni huko kisarawe mkoani Pwani.


Amesema CCM itakaposhinda na ataendelea kusimamia mapato ya halmashauri za mkoa wa Pwani ili kuimarisha kipato cha halmashuari ili ziwezekuendelea kutoa mikopo kwa akinamama, vijana na walemavu bila riba.


Amesema halmashauri nchini zimekuwazikitoa mikopo ambayo ni asilimia 10 ya mapato yake hivyo ili makundi hayo ya akinamama, vijana na walemavu wanufaike zaidi inabidi halmashauri nazo zisimamiwe kukusanya mapato yake ili fungu hilo la asilimia 10 la mapato liwe kubwa zaidi. 


Aidha Vulu amesema serikali inayoongozwa na CCM imefanya mengi katika sekta ya afya kwa kuimqarisha miundo mbinu, elimu na barabara hivyo ni sababu tosha kukipigia kura nyingi za kishindo ili kirejee madarakani kiendeleze mazuri iliyokwishaanza kuyafanya. 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana