Featured

    Featured Posts

MPEMBENWE: MKINICHAGUA NITAFUATILIA KITONGOJI CHA MBAWA KIPANDE HADHI

 Na Scolastica Msewa, Kibiti.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kibiti mkoani Pwani Twaha Mpembenwe ameahidi kuendeleza kufuatialia hatua za upandishaji wa hadhi ya kitongoji cha Mbawa katika kata ya Lualuke ili kiwe kijiji iwapo CCM itashinda na kupewa dhamana ya kuongoza.


Akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu katika kitongoji cha Mbawa ambacho tayali kimekwishaanza mchakato wa kupandisha hadhi ili kiwe kijiji.


Mpembenwe amesema kitongoji hicho kina kila sababu ya kuwa kijiji anachakua hiyo kero ili kwenda kuifanyia kazi mara baada ya uchaguzi mkuu ili zile huduma za msingi za kijiji zipatikane hapo hapo mbawa.


Amesema mchakato huo ni mrefu kwani huanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi ya wizara lakini baada ya ushindi wa CCM watashughulikia.


Amesema kitongoji hicho tayali kimekwisha fyatua tofari 2800 za ujenzi wa zahanati lengo lao likiwa kumaliza kero ya kutembea umbali mrefu wakifuata huduma za afya. 


Akizungumzia kero za vijana Mpembenwe amesema CCM itakaposhinda na ataendelea kusimamia mapato ya halmashauri za mkoa wa Pwani ili kuimarisha kipato cha halmashuari ili ziwezekuendelea kutoa mikopo kwa akinamama, vijana na walemavu bila riba.


Amesema halmashauri nchini zimekuwazikitoa mikopo ambayo ni asilimia 10 ya mapato yake hivyo ili makundi hayo ya akinamama, vijana na walemavu wanufaike zaidi inabidi halmashauri nazo zisimamiwe kukusanya mapato yake ili fungu hilo la asilimia 10 la mapato liwe kubwa zaidi. 


Aidha Mpembenwe amesema serikali inayoongozwa na CCM imefanya mengi katika sekta ya afya kwa kuimqarisha miundo mbinu, elimu na barabara hivyo ni sababu tosha kukipigia kura nyingi za kishindo ili kirejee madarakani kiendeleze mazuri iliyokwishaanza kuyafanya.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana