Featured

    Featured Posts

DK MAGUFULI ATAJA MAMBO MAKUBWA 28 ALIYOWAFANYIA WATANZANIA KWA MIAKA 5 YA UONGOZI WAKE


 Baadhi ya mambo muhimu yaliyosemwa katika mkutano wa Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM) na  Rais wa  Tanzania DK. JOHN POMBE MAGUFULI Mjini SINGIDA leo Septemba 1, 2020.

#TZS bilioni 470.4 zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Singida.

#Tumejenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.

#Hospitali 3 za wilaya zimejengwa katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.

#Katika kipindi cha miaka mitano viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa.

#Ajira milioni 6 zimezalishwa katika kipindi cha miaka mitano na katika kipindi cha miaka mitano ijayo tutazalisha ajira milioni 8

#TZS bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine.

#Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida iko hatua za mwisho kukamilika ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha sekta ya afya.

#Kulikuwa na Vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa  umeme mwaka 2015 lakini katika miaka mitano hii 2020 vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima.

#TZS bilioni 310 zimetumika kujenga miundombinu wezeshi.

#TZS bilioni 27.2 zimetumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.

#Uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.

#TZS bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa.

#Ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora imebaki km 20 kukamilika.

#Vituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima.

#Tunajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.

#Vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na Vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.

#Bajeti ya Wizara ya afya imeongezwa kutoka TZS bilioni 30 hadi TZS bilioni 270.

#Niko hapa kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama.

#Visima 4 virefu vimechimbwa kuongeza upatikanaji wa maji.

#TZS bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.

#Shule kongwe ikiwemo Mwenge Sec zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu.

#Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa TZS bilioni 850 hadi zaidi ya TZS Trilioni 1.5

#Tozo 114 zimefutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wamefutiwa kodi 54.

# tumeweza  kukusanya   tsh trioni1.5-1.9 kwa  mwezi  ukilinganisha na Bilioni  850 zilizokuwa zikiikusanywa hapo awali.

#Kwa mujibu wa ripoti ya  "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52  duniani kwa amani.

Mitandao ya simu imeimarika nchi nzima.

# Tumejenga ukuta wa km 25 eneo la Mererani ambao umesaidia  kudhibiti  wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.

#tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona kutokana  na maombi tuliyofanya kama taifa. Hii imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza

*Imeandaliwa na John Mapepele, PIO- Singida

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana