Kamati ya Maadili ya Mawakili imemwondoa Fatma Karume katika orodha ya mawakili Tanganyika kutokana na ukiukwaji maadili ya tasnia hiyo.
Taarifa zimesema, uamuzi huo wa Kamati ya Mawakili umefikiwa leo katika kikao chake kilichofanyika katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, huku sababu ikielezwa kuwa wakili huyo amekiuka maadili ya kazi yake kwa kiwango cha juu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu kutoa maamuzi ya kumsimamisha Fatma Karume kufanya kazi za Uwakili Tanzania bara na kuamuru apelekwe Kamati ya Maadili kwa madai ya kushambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Post a Comment