Mitano ya magufuli, Serikali imetekeleza miradi ya maji 1,423, ambapo miradi 1,268 ni ya vijijini na 155 ni ya mijini. Miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa ni mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Nzega, Tabora na Igunga; Mradi wa Maji wa Arusha pamoja na mradi wa kupeleka maji kwenye miji 28 unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 1.2. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali imeongeza upatikanaji wa majisafi na salama vijijini kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwaka 2020; na kwa mijini kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi asilimia 84 mwaka 2020. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali imeimarisha huduma za mawasiliano, hususan kwa kuboresha usikivu wa simu kutoka asilimia 79 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 94 mwezi Disemba 2019. Aidha, idadi ya watumiaji wa simu za mkononi pamoja na watumiaji data imeongezeka maradufu hali ambayo imechangiwa zaidi na kupungua kwa gharama za kupiga simu. *Acha kazi iendelee*
Mitano ya magufuli, Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa takriban kilometa 3,500 na hivyo kuifanya Tanzania iwe na kilometa 12,964 za barabara za lami. Barabara nyingine zenye urefu wa zaidi ya kilometa 2,000 zinaendelea kujengwa. *Acha kazi iendelee*
Mitano ya Magufuli, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi ya Tanzania, Serikali imejenga barabara za juu (flyover na interchange) Dar es Salaam ili kupunguza tatizo la msongamano wa magari, imekamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 13, likiwepo Daraja la Nyerere – Kigamboni, Daraja la Magufuli katika Mto Kilombero pamoja na Daraja la Sibiti. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali inaendelea na ujenzi wa madaraja mengine makubwa, likiwemo Daraja la Kigongo -Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2, Daraja la Salender lenye urefu wa kilometa 1.03 pamoja na Daraja la Wami lenye urefu wa meta 513.5. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, hakuna Mkoa au Wilaya ambayo haikupatiwa fedha za kujenga barabara za lami. Makao Makuu ya Mikoa na Wilaya karibu zote sasa zinang’ara kwa lami na taa za barabarani, ahadi ya kuunganisha Mikoa kwa barabara za lami nayo imetekelezwa kwa asilimia kubwa na kwa Mikoa ya Rukwa-Katavi, Katavi-Tabora, Singida-Tabora, Tabora-Kigoma na Kigoma-Kagera nayo inaendelea kuunganishwa. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mpanda – Tabora kilometa 359 na kukakimilisha ujenzi wa barabara ya Manyoni – Tabora, vilevile, inaendelea kujenga barabara ya kutoka Mpanda kwenda Kigoma na Kigoma hadi Nyakanazi zote kwa kiwango cha lami. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali inakamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa kilometa 300 na ujenzi wa Awamu ya Pili kutoka Morogoro hadi Makutupora umbali wa kilometa 422 umefikia asilimia 30. Ujenzi wa sehemu ya Mwanza – Isaka – Dodoma ipo kwenye maandalizi. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali imekarabati reli ya zamani kutoka Dar es Salaam hadi Isaka kilometa 970, imefufua usafiri wa reli ya Dar es Salaam –Tanga – Moshi – Arusha na imefanikiwa kurudisha tena usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga, Moshi hadi Arusha. Acha kazi iendelee
Mitano ya magufuli, Serikali imekamilisha Mradi wa Kinyerezi II, ambao umeiongezea nchi Megawati 240; na inakaribia kukamilisha upanuzi wa mtambo wa Kinyerezi I utakaozalisha Megawati 325 kutoka Megawati 150 za sasa. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali imeanza kutekeleza Mradi mkubwa wa Bwawa la Nyerere kwenye Bonde la Mto Rufiji. Mradi huu unagharimu shilingi trilioni 6.5 na utakapokamilika utazalisha umeme Megawati 2115, ambazo sio tu zitatuhakikishia umeme wa kutosha na wa gharama nafuu lakini pia utatusaidia kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi makubwa ya kuni na mkaa. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, Serikali imeendelea kutekeleza Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini, ambapo tumeongeza idadi ya vijiji vilivyofikishiwa umeme kutoka 2,018 mwaka 2015 hadi vijiji 9,112 mwezi Aprili 2020. Nchi yetu ina vijiji 12,268; hivyo tumebakisha vijiji 3,156 tu kufikisha umeme kwenye vijiji vyote nchini. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, idadi ya watumiaji wa umeme (energy access) imeongezeka kutoka asilimia 35 hadi asilimia 85. Na hii imechagizwa na ushushaji wa gharama za kuunganisha umeme kutoka shilingi 177,000 hadi shilingi 27,000. Acha kazi iendelee
Mitano ya Magufuli, tatizo la kukatikakatika kwa umeme limepungua, katika kipindi chote cha miaka mitano nchi yetu haikuwahi kuingia gizani. Acha kazi iendelee
Acha kazi indelee
Magufuli mitano tena
Ushindi kwa CCM
Post a Comment