Na Scolastica Msewa, Kibiti.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mama Gaudentia Kabaka amewataka wanawake nchini kuhakikisha wanachagua CCM katika uchaguzi mkuu ujao oktoba 28 mwaka huu kwani serikali ya CCM imeweza kutatua kero mbalimbali zinazomlenga mwanamke kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za Mgombea mwenza wa CCM Mama Samia Suluhu Hassan Mlandizi Kibaha mkoani Pwani Mama Kabaka amesema wanawake wa jumuiya hiyo pamoja na wanawake wote kwa ujumla wahakikishe wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwachagua wagombea wa CCM siku ya kupiga kura.
“Chagueni wagombea wa Ubunge, Udiwani na urais wa CCM ifikapo Oktoba 28 kwa kupiga kura CCM pia kwakuwa serikali ya awamu ya tano imeweza kuwakomboa wakina mama katika imeweza kutatua kero mbalimbali ambazo zinamlenga mwanamke kwa kiwango kikubwa”
Alisema “katika sekta ya Afya serikali ya awamu ya tano imesogeza huduma ya afya kwa kujenga hospitali za rufaa, hospitali, vituo vya afya zaidi ya 70 nchini kote na hospitali pamoja na zahanati lengo likiwa ni mwanamke asiende mbali kufuata huduma”
Alisema pia serikali imetoa mikopo mingi ya halmashauri na taasisi za fedha kwa wanawake, vijana na makundi maalumu ya walemavu na kuwasogezea huduma ya maji karibu na kumfanya mwanamke kutotembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo.
Alisema pia imefuta ada za shule za msingi na sekondari kero iliyokuwa ikimgusa moja kwa moja mwanamke.
Mgombea Ubunge wa jimbo la kibiti Twaha Mpembenwe ameomba serikali isaidie fedha za ujenzi wa bara bara Kwa kiwango cha lami bara bara ya kilomita 99 kuanzia Kibiti hadi kwenye mradi wa umeme Wa mwalimu Julius kambalage nyerere huko kwenye mto Rufiji ili wananchi Wa vijiji vilivyopembezoni waweze kukuza uchumi.
Hata hivyo Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassani alisema serikali lazima itatengeneza hiyo bara bara Kwa kiwango cha lami maana serikali imekwisha wekeza fedha nyingi kupitia mradi huo.
Post a Comment