Na Scolastica Msewa, Kibiti
Mgombea wa Ubunge jimbo la kibiti mkoani Pwani Twaha Mpembenwe amesema amani iliyopo sasa hivi wilayani kibiti ni sababu tosha ya wanannchi wa jimbo hilo kumchagua Mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa kura zote za ndio asilimia 100.
Amesema hayo katika uzinduzi wa kampeni jimbo la kibiti kwa tiketi ya CCM katika kata ya Mwambao ambapo mwenyekiti Wa UWT Mkoa Wa Pwani Farida Mgomi alikuwa Mgeni rasmi.
Mpembenue amesema miezi kadhaa iliyopita wilayani humo maisha yakuwa mazuri sana ya amani na utulivu kwa kuku lakini haikuwa hivyo kwa binadamu kwani kuku ndio waliokuwa na uhuru wa kutembea muda wote kwa uhuru na amani lakini sio kwa binadamu lakini Mgombea Urais kwa jitihada zake leo kibiti ipo huru ina amani na utulivu.
“Mpembenwe amesema suala la amani na utulivu katika jamii ni jambo kubwa sana na la msingi sana hivyo amewakata wananchi wa jimbo la kibiti kumuenzi kwa kumpigia kura nyingi za kishindo Dr. John Pombe Magufuli maana ndiye alisimamia hadi amani na utulivu vimerejea Kibiti alisema Mpembenwe.
Amesema jitihada alizofanya kurudisha amani na utulivu kibiti wananchi wanazijua, wana CCM wanazijua, wapinzani nao wanazijua na watanzania wote kwa ujumla waliziona na wanazijua hivyo hakuna wakupinga amani na utulivu uliopo kibiti ni kutokana na jitihada za Mgombea huyo wa Urais.
"Naomba sana vijana wenzangu, wazee wangu, amani sio jambo la kuchezea tuilinde na kuitunza amani yetu" alisema Mpembenwe.
Aidha akizungumzia fedha nyingi zilizoletwa wilayani humo Mgombea Ubunge huyo ameishukuru mno serikali ya awamu ya tano ambayo ilimepeleka zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo fedha ambazo ni nyingi haijawahi kutokea.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya kibiti Jabil Malombwa amewataka wenyeviti wa vitongoji wa CCM, wenyeviti wa Vijiji na wajumbe wa nyumba kumi siku ya terehe 28 mwezi oktoba wahakikishe kila mmoja anatoka nyumbani kuelekea kwenye vituo vya kupiga kura ili kila aliyejiandikisha kupiga kura akapige kura bila kukosa.
Post a Comment