Mlinzi wa Brazil Alex Telles, 27, anataka kuondoka klabu ya Porto na kujiunga na Manchester United, ambao wanajaribu kushawishi kupunguziwa dau lake la £36.6m. (Telegraph - subscription required)
Liverpool wanatazamiwa kumtumia mshambuliaji Sadio Mane kumshawishi mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Senegali Kalidou Koulibaly ili atue klabuni hapo kutoka Napoli, licha ya Manchester City na Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29. (Le Parisien, via Sun)
PSG wanamtaka beki wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27, kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail)
Roma wanatarajiwa kuweka ofa nyingine ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling, 30, ambaye aliichezea timu hiyo ya ligi ya Serie A kwa mkopo msimu uliopita. (Guardian)
Atletico Madrid wanalenga kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 23. (Mundo Deportivo - in Spanish)
West Ham wako tayari kupambana na Manchester United kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati wa Swansea City na Wales Joe Rodon, 22. (Guardian)
Wrexham imetengaza ofa kutoka kwa mmiliki mpya - nyota wa Hollywood, Ryan Reynolds
West Ham United imeweka ofa yenye thamani inayofikia £33m kwa ajili ya mlinzi wa kati wa Saint-Etienne Wesley Fofana (19), ambaye anawaniwa pia Leicester City. (Sky Sports)
Burnley wako kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili winga wa wekundu hao na Wales, Harry Wilson, 23. (Independent)
Lazio imefikia makubaliano na Southampton kwa ajili ya mlinzi wa Uholanzi, Wesley Hoedt, 26, kurejea kwenye klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Sky Sport Italia - in Italian)
Barcelona na Bayern Munich zimeweka ofa ya kumsajili Mlinzi wa kulia wa Ajax na Marekani Sergino Dest, 19. (Marca)
Bayern imewasiliana na Mario Gotze kuhusu kujiunga tena na klabu hiyo. Mshambuliaji huyo wa Ujerumani, 28, ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport Bild - in German)
Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid na Colombia Santiago Arias, 28, amewasili Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na Bayer Leverkusen. (Marca)
Mshambuliaji wa zamani wa Italia Francesco Totti anatarajiwa kurudi Roma kama mkurugenzi wao mkuu wa michezo. (Corriere dello Sport - in Italian)
Post a Comment