Featured

    Featured Posts

TUSHIKAMANE NA DK. MAGUFULI, GADAFFI WETU WA TANZANIA.

Rais Dk. Magufuli ambaye anagombea tena Urais miaka mingine mitano
'African Unity' ndio ulikuwa kama wimbo wa kila siku  wa Kanal Muammar Gadaffi kwa Waafrika kwa sababu alipenda sana Afrika iwe moja na Waafrika wawe wamoja. 


Hapana shaka kwamba hadi anaingia kaburini Gadaffi bado aliamini katika Muungano ambao ungewafanya Waafrika wasionewe, wasinyonywe, wasibaguliwe yaani wawe imara kiuchumi  wasibabaishwe na Mataifa mengine.


Gadaffi alizaliwa katika familia ya kimaskini ambao walikuwa wakitegemea kuchunga farasi ili waweze kuishi lakini pamoja na kuwa katika familia yenye dhiki kubwa alikuwa na ndoto ya kulikomboa taifa la Libya.


Gadaffi baada ya kufanikiwa kuwa Rais kwa kufanya Mapinduzi bila kumwaga damu, watu wa Libya waliishi Kama wako peponi.


🖊️Vijana walijengewa nyumba buuure na serikali hata bili ya umeme walilipiwa na serikali.


✍️ Wakiugua walitibiwa bure ndani na nje ya Libya.


✍️Wakitaka kuoa serikali ya Gadafi ilikuwa inawalipia

 mahari na kuwapa pesa za kuanzia maisha.


✍️ Kijana akipata mtoto Serikali ya Gadaffi inamuongezea pesa zingine.


✍️ Akitaka Gari serikali ilikuwa inawalipia nusu ya gharama za kununua gari.


✍️ Waliohitimu vyuo na kukosa ajira walikuwa wanalipwa sawasawa na walioajiriwa.


✍️ Serikali ilikuwa ikiuza mafuta ilikuwa inagawana pesa na wananchi wake. Yaani unaenda kwenye akaunti unakuta mipesa imejaa!


✍️Pamoja na Libya kuwa jangwa, Gadaffi alitengeneza mto na kuanzisha kilimo Cha umwagiliaji.


✍️Wananchi wa Libya walitakiwa kuonesha nia tu ya kulima na vitendea kazi vyote walipewa bure.


Lakini pamoja na kufanya hayo yote bado walimwona Gadaffi hafai baada ya kuhadaiwa na mabeberu walioimezea mate Libya. 


Mabeberu waliwatumia baadhi ya Walibya wenye uchu wa madaraka, wakajaza maneno ya fitna ikiwa ni pamoja na kuwaambia maneno ya ghiliba.


 Wakawaambia " Hivi mnavyoona Gafaffi anawafanyia mnadhani anawapenda? hawapendi anawafanyia hivyo ili mwendelee kupumbazika, anavyowapa ni kidoogo sana kuliko anavyojipa yeye.


 Mkimuondoa madarakani mtaishi maisha yaliyo bora zaidi kuliko hivyo mnavyohudumiwa kama mifugo!"


Baadhi ya Walibya wenye uchu wa madaraka ambao walikubali kuwa vibaraka wa Mabeberu wakaingia mitaani kuingiza propaganda hiyo chafu, wakaghilibu akili za wenzao, wakaingia mabarabarani kuandamana.


Serikali ilipojaribu kutuliza maandamano ili nchi iwe shwari, Mabeberu wakaibuka na kuingia Libya kwa kisingizio kwamba Serikali inawaonea wananchi, eti inanyima demokrasia, inawanyima wananchi wake haki ya kuandamana!


Hatimaye vibaraka au mapandikizi yalipata nguvu, ma hafuko yakawa makubwa hadi Gadaffi wakammiminia risasi, wakamvua nguo, wakamburuza barabarani na kisha kumtundika kwenye bucha ili kila mmoja amwone hadi alipoanza kuoza.


Libya ilivurugika, maisha ya Wanalibya yakaharibika,

Neema zote walizokuwa wanapata zikayeyuka, furaha yao ikayeyuka pia.


Hadi sasa Libya haijatengemaa, ikatulia, machafuko hayaishi. Dhambi ya usaliti inazidi kuitafuna Libya.


Sasa, kiongozi wetu Rais Dk. John Pombe Magufuli ni Gadaffi wa Tanzania. Anao uchungu na Tanzania yenye neema, anawapenda Watanzania. Anatamani siku moja aone Watanzania wakifaidi matunda ya utajiri wa nchi yao Tanzania. 


Lakini kama ilivyo desturi ya Mabeberu tayari yameshaweka mapandikizi yake yenye kuwa tayari kuisaliti nchi yao Tanzania kwa ajili ya uchu wa madaraka na kumiliki mali binafsi.


Mapandikizi hayo tayari yameahaonekana. Lakini Watanzania tuna jambo moja tu, kuwa kitu kimoja kwa kuyakataa mapandikizi haya kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote. Watanzania tumeshaona mfano kwa Waafrika wenzetu wa Libya, kamwe isitokee kwetu.


Na njia ya kuonyesha kuwapuuza Mabeberu na vibaraka au mapandikizi yao, Siku ya Jumatano ya Oktoba 28, meaka huu huu wa 2020, twendeni vituoni sote, tukiwa na jambo letu moja tu, nalo siyo lingine ila kumpigia kura za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM. Hii itatoa ishara kuwa hatutaki mapandikizi.


Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake.


Imeandikwa na Kalam ya Audax na kuhaririwa na Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana