Featured

    Featured Posts

THE CAPITAL PARK KIOTA ZA MARAHA KILICHOZINDULIWA JIJINI DODOMA

Mambo yameiva jijini Dodoma, baada ya The Capital Park kioo cha maraha kuzinduliwa Iringa Road mkabala na Nala ambapo kuna kila aina ya starehe. Mahali hapo unaweza kupata huduma za kila aina zitakazokufanya uondoe uchofu baada ya majukumu yako ya kila siku.

 Pia eneo hilo linaweza kukuondolea Stress kwa kuangalia matukio mbalimbali ikiwemo michezo kupitia Screen 11 zilizosambazwa kila kona ya eneo hilo. Pia kuna Counter za kisasa zilizosheheni vinywaji vya kila aina. 

Vilevile pana jiko la kisasa lenye vyakula vya kila aina pamoja na nyama choma za mbuzi, kuku, ng'ombe na michemsho. The Capital Park ina eneo kubwa la kuegesha magari na vyombo vingine vya moto vyote  huku vikilindwa na vijana maalumu ili kumhakikishia usalama mywaji.

 Vile vile kuna wahudumu wanaopokea wateja kwa bashasha  na kuwapatia huduma kwa haraka. Nje kuna huduma ya Taxi, Bajaji na Bodaboda waliovalia vijaketi vyenye jina la  The Capital Park.
Ukiwa kwenye kiota hicho utaburudishwa na muziki poa unaoporomoshwa na Ma DJS  Jab na Eddo.
Moja ya Counter za kisasa ikiwa imesheheni vinywaji vya kila aina. Counter hiyo ina Screen nne ambapo kila upande alipokaa  mteja anaweza kuangalia tukio.



Wateja wakila bata




Jiko la Kisasa lililopo katika kiota hicho maridhawa




 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana