Featured

    Featured Posts

TOUFIQ: WANAWAKE TUTAWASHAWISHI WAUME ZETU WOTE WAMPIGIE DK MAGUFULI KURA NYINGI APATE USHINDI WA KISHINDO

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dk. John Magufuli (wa pili kulia), akiwa na viongozi wenzie wakifurahi baada ya Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Fatuma Toufiq  (kushoto) kuahidi kwamba yeye na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma watafanya kampeni kwa kuwashawishi waume zao ili ifikapo Oktoba 28, mwaka huu kuhakikisha wote wanampigia Dk. Magufuli kura apate ushindi wa kishindo.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Jumamosi  Oktoba 29, 2020, alisema pia watawashawishi watoto wao, vijana, marafiki na jamaa pamoja na wananchi  wampigie Dk. Magufuli kura nyingi za ndiyo. Viongozi wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa  CCM, Dk. Bashiru Ali, Makamu Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Fatuma Toufiq akiingia jukwaani kujinadi yeye pamoja na wagombea wengine wa CCM na hasa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli (Wa pili kulia).  Wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa  CCM, Dk. Bashiru Ali, Makamu Mwenyekiti, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk.  Hussein Ali Mwinyi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Toufiq ambaye pia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni na kuongoza kura za maoni za ubunge Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa CCM  (UWT) Mkoa wa Dodoma, akiendelea kunadi ili wananchi wawachague wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.












 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana