Featured

    Featured Posts

WANAWAKE MSIDANGANYIKE MPIGIENI KURA DK MAGUFULI ANAYETUTHAMINI-OKASH



Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mpwayungu, Jimbo la Mvumi, Anthony Sakalani.


Okash akimuombea kura kwa unyenyekevu Sakalani
Okash (wa pili kushoto) akimwaga sera za CCM  katika kikao maalumu cha kampeni katika Kata ya Mpwayungu.


Na Mwandishi Wetu, Mvumi.

MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash amewasihi wanawake waache kudanganyika bali wasimame imara kulinda kura zao kwa kumpigia mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli ambaye anawathamini.


Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni kwenye kampeni za CCM katika Kata ya Mpwayungu, Jimbo la Mvumi, ambapo alimnadi Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Anthony Sakalani.


"Nawasihi wanawake wenzangu msimame imara msije mkadanganyika, kura zenu ndiyo mkombozi wetu, tumpeni Dk. Magufuli ambaye ametuthamini mno hasa kwa uamuzi wake wa kumteua mwananmke mwenzu Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wake wa urais,"amesema Okash huku akishangiliwa.


Amesema kuwa, Dk. Magufuli amemteua tena Mama Samia ambaye ameonesha ujasiri wa uchapakazi katika miaka mitano akiwa Makamu wa Rais katika Serikali yake ya Awamu ya Tano. "Hakika Mama Samia ameonesha dhahiri kwamba wanawake tukipewa nafasi tunaweza," amesema Okash. 


Okash, mwanamke mpambanaji ambaye licha ya kuzisaka kura za wagombea wa CCM katika vikao vya ndani, mikutano ya kampeni  lakini vile vile amekuwa akizitafuta katika vijiwe vya kahawa, kwa Mama Lishe, sokoni, salon na vikundi mbalimbali vya akina mama. 


Anapokwenda maeneo hayo, Okash amekuwa akitangaza zera za CCM, mafanikio  ya Serikali ya Awamu ya Tano  inayoongozwa na Dk Magufuli, lakini pia amekuwa akiwaelea mazuri yaliyomo kwenye Ilani ya chama hicho yatakayoanza kutekelezwa mara baada ya CCM kupata ridhaa ya kupigia kura nyingi na wananchi.


 

 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana