*Awambia wakimpelekea Tulia moyo wake utatulia,Mbeya imechelewa sana
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mbeya
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewaomba maelfu ya wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini kuhakikisha katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu wanamchagua Dk.Tulia Ackson kuwa mbunge wa jimbo hilo ili kuleta maendeleo ambayo yamechelewa kutokana na kukosekana mtu wa kuyapigania.
Akizungumza leo Septemba 30 mwaka huu wa 2020 katika viwanja vya Uwanja wa Ndege wa zamani , Dk.Magufuli amesema leo ni siku muhimu kwa mkoa wa Mbeya huku akifafanua tangu alipoingia Mkoa wa Iringa hadi anafika mkoa huo amekutana na makundi ya watu wengi."Nimefanya mikutano zaidi ya 20 na hata hapa nimechoka kweli,watu wamesimama tangu asubuhi wananisubiri.
"Makaribisho haya ambayo nimeyapata Mbeya ni makubwa sana , ahsante , mmeacha historia na mmeandika historia katika maisha yangu, narudia kusema Mbeya sitawaangusha.Ndugu zangu mwaka 2015 tulipita hapa kuomba kura, Mbeya mlitusikiliza na natambua nilipata kura nyingi lakini kwa mbunge mkasema hapana, niseme kwa dhati nilisikitika lakini sikuwachukia.
"Sababu za kushindwa zilitokana na CCM wenyewee, nilichofanya kuhakikisha Mbeya haitoki kwenye ramani, niliamua kumtafuta mama mmoja msomi anayeitwa Dk.Tulia, nikamteua kuwa Mbunge ili yale ambayo yatajitokeza kwa ajili ya Mbeya awe anasemea na ananyota kali baada ya kumteua tu akawa Naibu Spika wa Bunge,"amesema Dk.Magufuli.
Amesema kuwa Dk.Tulia Ackson amekuwa amkimsumbua kuhusu maendeleo ya Mbeya."Na kwasababu leo umekuja mwenyewe, sitakuteua tena kuwa Mbunge wa kuteuliwa. Nimeamua kukuleta kwa ndugu zako wakusubu kwa kazi zako nzuri, naamini kwa umati huu mtaniletea Dk.Tulia awe mbunge wa hapa.
Amesema wananchi wa Mbeya Mjini katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 waliamua kuchagua wasanii."Mlikosa wasemaji mkapata wasanii wa kuwadanganya, sio wasanii wazuri kama akina Diamond na Ali Kiba, naomba mniletee Tulia, nawaomba mniletee Tulia , ndugu zangu Mbeya nawapenda na ukipendwa pendeka.Nataka niwaeleze ukweli msijichelewe, naomba wana Mbeya wa vyama vyote kwenye katika maendeleo hakuna chama, maendeleo ni maendeleo.
"Nataka kuibadilisha Mbeya kabla ya muda wangu haumalizika , nataka Mbeya isiwe eneo la usindikizaji, naomba sana wana Mbeya kwa upendo mkubwa tusirudie makosa.Tunahitaji mandeleo haya yote na bahati nzuri linakuwa Jiji kubwa, idadi ya watu sasa imefikia milioni tatu.Jiji la Mbeya lina Wilaya moja, Sugu namuomba kura yako, tunataka maendeleo , tunataka kuijenga upya Mbeya, nataka muwe na wabunge ambao wakiwa bungeni wakati wa kugawana kasungura kadogo nao wapate, tunataka kuibadilisha Tanzania, wakati wa kubishana umepitwa na wakati.
"Wana CCM wenzangu shikamaneni kuhakikisha Dk.Tulia anakuwa Mbunge wa hapa Mbeya Mjini.Niwaomba wafanyabiashara wa Mbeya , watani zangu Wakinga na wengine wote nileteeni Tulia, nileteeni Tulia moyo wangu utatulia, nataka ndugu zangu wana Mbeya nikija niwe naona raha na huu ndio ukweli na kama nilimteua siku mbili tu akawa Naibu Spika ana nyota ya maendeleo, Mbeya tuwe kitu kimoja, tumejichelewesha vya kutosha, mimi ni mtoto wenu, mtumishi wenu, ndio maana nimekuja kuwapa huu ujumbe, wapo wanaosema huyu ni mwanamke, kuwa mwanamke mwanamke ni dhambi?
"Nileteeni Tulia, nileteeni Tulia, narudia wana Mbeya nileteeni Tulia.Nikuombe Tulia utakapoteuliwa kuwa mbunge wa Jimbo hili watumikie watanzania wote, Mbeya imechelewa , wana Mbeya tubadilike tunahitaji maenedeleo zaidi , nina omba mniletee madiwani wa CCM ili fedha ambayo tutazipanga hapa zitumike kuleta maendeleo.
"Nataka kikao cha kwanza kama watakuja wa CCM, wakija wengine wasiniulize, kikao cha kwanza kiwe kujadili namna ya kuigawa Wilaya na Mbeya kuwe na wilaya mbili, kwa hiyo mkakae namna ya kuligawa Jiji hili, moyo wangu uko kwenye Jiji hili,"amesema Dk.Magufuli.
Post a Comment