Featured

    Featured Posts

HAKUNA VITUO HEWA VYA KUPIGIA KURA NCHINI -DKT.MAHERA

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa  katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera ,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama kutangaza kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura nchini vimeongezwa.

………………………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchin (NEC) imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna vituo hewa vya kupigia kura vimeongezwa katika baadhi ya majimbo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera,amesema kuwa hakuna vituo hewa vya kupigia kura nchini huu ni upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wa siasa kutangaza kuwa kuna vituo hewa.

”Nashangaa kuona taarifa za uzushi zikisambaa kwenye mitandao na baadhi ya viongozi wa vyama kuanza kulalamika na kuzusha kuwa NEC imeongeza vituo hewa vya kupigia kura nchini”amesema Dkt.Mahera

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana