Featured

    Featured Posts

KAMPENI ZA LALA SALAMA ZAZIDI KUCHANJA MBUGA JIMBO LA TEMEKE


Abbas Mtemvu akimnadi Mgombea Udiwani Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Alhaji Uzairu Athumani (kushoto), wakati wa kampeni hizo zilizofanyika Kata ya Tandika Oktoba 25 Dar es Salaam.



Diwani Viti Maalum Kata ya Tandika, Mariam Mtemvu akiwapungia mkono Wanachama na Wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa Kampeni Uliofanyika Octoba 25, 2020 wakati alipokuwa akijumuika na wanachama kuchena nao



Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Abbas Mtemvu alipo kuwa Akimnadi Mgombea Udiwani Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Alhaji Uzairu Athumani (pichani hawapo), wakati wa kampeni hizo zilizofanyika Kata ya Tandika Oktoba 25 Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama 

Mgombea Udiwani Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Alhaji Uzairu Athumani (katikati) akisindikizwa na baadhi ya viongozi na msururu wa wanachama na wananchi wakati akiingia katika Mkutano wake wa Kampeni Uliofanyika Kata ya Tandika Octoba 25, 2020 Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tandika, akizungumza jambo ambapo alianza kwa kutoa salamu ya Mungu  na alisema, Ndugu viongozi wa Chama na kwa wanachama na wananchi , kazi yangu ni moja tu nayo ni kufungua mkutano nipate kuwaachia wenyemkutano wamwage sera

Tukiwa katika mwendelezo wa Kampeni za uchaguzi wa Udiwani leo simsemaji na mezakuu imeenea hivyo neno langu kuu nikuwaomba kura kwa ajili ya Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani wote nawaombea kura   


Mbunge Mstaafu Viti Maalum Jimbo la Kondoa Asha Ngede akiwaasa Wananhi na Wanachama kuwachagua viongozi wote wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani upinzani hakuna kitu.



Mgombea Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Temeke, Alhaji Uzairu Athumani (kulia) akiteta jambo na Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa Kampeni za lala salama zinazoendelea Jimboni humo











Abbas Mtemvu akiwaomba wanachama na wananchi wote kutofanya makosa katika Uchaguzi huu utakaofanyika hivi karibuni kwani kipimo kikubwa ni gonjwa la CORONA kitu ambacho Nchi za wenzetu mpaka leo wanajifungia ndani na Rais wetu angesema tujifungie ndani hadi leo tungekuwa hali gani? alihoji Mtemvu

Kwani wengine tungekufa na wengine akina Mtemvu tungetoka vitumbo hatuna, wengi Watanzanai tukitoka ndio tunarudi na chakula majumbani mwetu naomba kura zote tumpe Mhe. Rais wetu mpendwa Magufuli, Wabunge wetu na Madiwani.

Hatuna shaka na Rais wetu Mpendwa mchapa kazi na hakuna asiyemjuwa na yote ili ayakamilishe yaliyomoyoni mwake nukumpa Wabunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi kwani amejipanga kuwahudumia wana Tandika na Watanzania kwa ujumla ndio maana nikasema nawaombeni tucheke wote kwani kunasura nazijuwa

Nawaombeni mjuwe Siasa ni Maisha na tusikubari kupoteza Diwani kumpoteza Mbunge na kupoteza Rais imetokea 2005 hatahivyo namshukuru Rais na imeandaliwa pesa nyingi kwa ajili ya Dar es Salaam 


Nina uhakika tukimpa Dorothy Kilave na Diwani Uzairu  kwa yale tuliyoyapanga ndani ya miaka mitano yatafanyika Tandika na mtashangaa nasisi bado tupo Wabunge Wastaafu hatutokaa mbali kwani kunamiradi tukiona hatujapata tunambunge na tuna Diwani tutawakumbusha


Wafanya Biashara mkawaambie Siasa ni maisha na kazi yetu ni kumchagua Rais wetu Magufuli, Mbunge wetu Dorothy Kilave na Madiwani wetu watayafanya mengi ikiwemo kituo cha mabasi




Abbas Mtemvu akimnadi Mgombea Udiwani Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Alhaji Uzairu Athumani (kulia), wakati wa kampeni hizo zilizofanyika Kata ya Tandika Oktoba 25 Dar es Salaam.

 Mgombea Udiwani Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Alhaji Uzairu Athumani akiwahakikishia wakazi wa Kata ya Tandika na vitongoji vyake kuwa changa moto zao anazifaham na anaomba kura za Rais Magufuli na Mbunge wake  Dorothy Kilave aende kuzitatua mara moja na kuwatengea mikopo wafanya Biashara na huku akiwaonesha kitabu cha Ilani ya Chama hicho . 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana