Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akiwa katika kikao kuhusu mwitikio wa wananchi kuhusu mradi wa maji wa Kemondo na Burhan Mohammed, Mtendaji wa Kijiji cha Rwagati (katikati) na Cyriacus Sosthenes, Mtendaji wa Kata ya Kemondo (kulia). Kushoto ni Mhandisi Lyidia Joseph, Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Huduma ya Maji wa Wizara ya Maji.
Mfanyabiashara ya Samaki, katika kambi ya mabanda ya uvuvi-Kemondo, Bi. Christina Wangwi, akitoa maoni yake kuhusu mradi wa maji wa Kemondo ambapo ametoa maoni ya kuongezewa muda zaidi kuwezesha kuhamisha vifaa katika eneo la ujenzi wa chanzo cha maji na kuhamia katika eneo mmbadala ambalo limeshaandaliwa kwa shughuli hiyo ya kuuza samaki.
Ujenzi wa mabanda ukiendelea katika eneo jipya lililoandaliwa kwa ajili ya mabanda ya kambi ya uvuvi Kemondo. Eneo jipya limeanzishwa ili kupisha utekelezaji wa mradi wa maji na kuepuka uchafuzi wa maji kuzunguka eneo la chanzo
Post a Comment