Jeshi la Polisi linamshikilia Stella Kangoza (29) kwa kumchoma moto mikononi binti yake mwenye miaka 9 akimtuhumu kumuibia Tsh. 400 aliyopanga kutoa sadaka Kanisani.
Binti huyo anasoma Darasa la 3 katika Shule ya Msingi Chemchem iliyopo Manispaa ya Sumbawanga. Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Justine Masejo amesema, kitendo hicho ni cha kikatili na Mama huyo amemsababishia binti yake ulemavu.
Kwa sasa, binti huyo amelazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa awali wa Shauri lake kukamilika.
Kamanda Masejo amewaonya wananchi hasa Wazazi wanaotumia nguvu kutoa adhabu kwa watoto wao.
Post a Comment