Na Scola Msewa, Pwani
Mgombea ubunge viti maalum kwa tiketi ya CCM mkoa Pwani Subira Mgalu amewaomba wananchi wa mkoa Pwani kuwapigia kura wagombea wote wa CCM kwa kuwa Serikali yake ya awamu ya tano muhula wake wa kwanza imefanya mapinduzi makubwa katika maendeleo ya watu na vitu.
Subira ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni za kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli katika Kijiji cha Lugoba Kata ya Lugoba ambapo Diwani wa Kata ya Lugoba.
Amesema serikali ya CCM yenye nia ya kuandaa mazingira wezeshi kufungamanisha na Uchumi jumuishi na uchumi wa mtu mmoja hali iliyopelekea Nchi yetu kuingia Uchumi wa Kati Miaka mitano kabla ya muda uliotarajiwa ambao ni 2025.
Subira akitolea mfano maendeleo ya Vitu yaliyofanyika kwenye Kata ya Lugoba na Mkoa wa Pwani kwenye Sekta za Miundombinu, Maji, Nishati, Elimu Mawasiliano, Afya.
Subira akirejea pia kwenye historia vitabu vya Dini juu ya namna Mwenyezi Mungu alivyofanya kazi yake Takatifu ya uumbaji aliumba kwanza Dunia yenye Ardhi na miti kisha akamuumba Adamu na Hawa na kuwapeleka kwenye Bustani ya Aden kumaanisha kuna umuhimu mkubwa wa Maendeleo ya Vitu kwanza katika kuleta maendeleo ya watu .
Amewataka Wananchi wa Lugoba kuwapuuza wapinzani wanaobeza Maendeleo makubwa ya Vitu katika sekta mbalimbali yaliyosimamiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano .
Aidha Subira amewahimiza Wananchi kutunza shahada zao za kupigia kura na kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la uchaguzi Tarehe 28/10/2020 na wasipoteze kura zao kwa Wapinga maendeleo .
Post a Comment