Akitangaza matokeo ya kura zote, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, leo Oktoba 30, 2020, alimtangaza Dk. Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupata kura milioni 12.516 (12,516,252) sawa na asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.
Kwa mujibu wa Kaijage, waliokuwa wagombea wa vyama vingine na kura walizopata ni Bernard Membe (ACT- Wazalendo), kura- 81,129, Profesa Ibrahim Lipumba wa (CUF), kura -72885, Yeremia Maganja (NCCR) aliyepata kura - 19969, Khalifan Mazurui (UMD), kura - 3721, Cecilia Mmanga (Makini), kura - 14556.
Wengine ni Muttamwenga Mgaywa (SAU), Kura-14922, Twalib Kadege (UPDP), kura - 6194, Seif Maalim Seif (AAFP), kura - 4635, Queen Sandiga (ADC), kura - 7627, Hashim Rungwe (CHAUMMA), kura-32,878, John Shibuda (Ada Tadea), kura- 33,086, Leopold Mahona (NRA), kura - 80787 na Philipo Fumbo (DP) - 8283
Kufuatia ushindi huo wa kishindo Dk. Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM anaingia katika awamu yake ya pili ya uongozi, baada ya awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 2015 na kumalizika 2020 sasa ataendelea kwa kipindi cha 2020 hadi 2025.
Mbali na wa Dk. Magufuli kuibuka mshindi, CCM pia imefanikiwa kuzoa viti vingi kupindukia vya Udiwani na Ubunge katika uchaguzi huo ulijumuisha majimbo 264 nchini ambapo kwa Tanzania Bara vyama vya upinzania vimeamabulia viti viwili vya Ubunge kwa Chadema kushinda Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa na Cuf kushinda jimbo la Mtwara Vijijini.
Katika Uchaguzi huo, dalili za CCM kushinda kwa kishindo zilionekana mwanzoni mwa mchakato ambapo katika wagombea wote wa Ubunge wa vyama vyote 14, waliokuwa 1254 kati yao 28 wa CCM walipita bila kupingwa huku madiwani 873 wa CCM nao wakipita pia bila kupingwa
Katika Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020, jumla ya watu 15,91950 walipiga kura wakiwa ni kati ya watu 29,754,699 ambao kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) walijiandikisha kupigakura.
Post a Comment