Rais Dk. Magufuli akiwa na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu Hassan
Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu wanatarajiwa kukabidhiwa rasmi Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais siku ya kesho Novemba 1,2020.
Hafla hiyo ya Makabidhiano inatafanyika kesho Jumapili kuanzia saa moja asubuhi katika Ofisi za Jengo la Uchaguzi House lililopo Njedengwa jijini Dodoma.
Dkt.Magufuli alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jana kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi mno wa kura 12,516,252, akifuatiwa na Tundu Lisu wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) mwenye kura 1,933,271 huku Bernard Membe kutoka Chama cha ACT-Wazalendo akiwa amepata kura 81,129.
Ushindi wa Dkt.Magufuli umepatikana baada ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu uliofanyika October 28,2020 huku jumla ya waliojiandikisha ni 29,754,669, na kura halali zilizopigwa ni 14,830,195 huku kura 261,755 zikikataliwa.
Baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Rais Mteule Dkt.John Magufuli na Makamu wake watasubiri kuapishwa rasmi
Post a Comment