…………………………………………………………………………………….
Katika kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, Benki ya NMB kupitia Mameneja wake wa huduma kwa wateja wa Kanda ya Dar es Salaam, Nyanda za Juu na Kanda ya Ziwa imetoa vifaa mbalimbali vya Afya vyenye thamani ya sh. milioni Tisa, katika mikoa ya Iringa na Kagera ikiwa ni sehemu ya kurudusha kwa jamii.
Mbali na vifaa hivyo, wafanyakazi wa NMB Tawi la Iringa wametoa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi Mapinduzi, Wilolesi na Saint Dominic na baadae kuwapa wanafunzi wa shule hizo elimu juu ya masuala ya kifedha.
Katika Mkoa wa Iringa, vifaa vilivyokabidhiwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni; mashuka, vitanda vya kujifungulia kwa akina mama, na vitu mbalimbali kama pampasi, mafuta ya kujipak na sabuni kwa ajili ya watoto.
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Ziwa Baraka Ladislaus, alisema kuwa NMB imechangia vifaa vya shilingi milioni 25 tangu mwezi Januari mwaka huu kwa ajili ya kuboresha huduma za afya Mkoani Kagera kama sehemu ya jitihada za benki hiyo kuunga mkono hatua za Serikali za kuboresha sekta ya afya nchini.
Akipokea vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Bandiati Gangole alisema kuwa msaada huo utapunguza adha iliyowapata wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na sehemu ya wajawazito kujifungua ambayo kabla ya msaada huo haikuwa na kitanda chochote.
Post a Comment