KATIBU wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mambo mbalimbali yakiwemo mwenendo wa kampeni za uchaguzi za CCM pamoja na maandalizi ya Mkutano wa kampeni utakaofanyika Octoba 3,mwaka huu katika viwanja vya Maisara Mnazi Mmoja Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli. (PICHA NA IS-HAKA OMAR ZANZIBAR)
***************************************
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) RAIS Dk.John Magufuli, anatarajiwa kuwahutubia Wana CCM na Wananchi kiujumla katika viwanja vya Mnazi mmoja mjini Unguja ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kunadi sera za Chama cha Mapinduzi(CCM).
Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Taifa, Humphrey Polepole ameyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za Chama cha Mapinduzi kisiwandui Mjini Zanzibar.
“Siku ya kesho (leo) katika viwanja vya Mnazimmoja tuna jambo letu wazanzibar na watanzania kwa ujumla, tutakuwa na mkutano mkubwa wa kampeni za mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kipenzi cha watu, mpenda maendeleo, mtetezi wa wanyonge, wapinzani wakimuona wanatoka mbio si mwengine ni DK. Magufuli,” alisema.
Polepole alisema, kesho (leo) wazanzibar wanataka kuona na kusikia maono ya
wagombea wao, wa Tanzania bara na Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi ya
kuipeleka Tanzania mbele.
“Kesho (leo) tutasikia ustawi wa maendeleo, miundombinu ya kiuchumi, tunataka kusikia maisha ya watu yani kesho itakuwa ni yajayo yanafurahisha, hivyo iwakaribishe sana watanzania wenzangu wa zanzibar wote kutoka Unguja na Pemba katika viwanja vya Mnazimmoja tukasikilize maono ya Magufuli,” alisema.
Alisema watanzania watapata nafasi ya kusikiliza maono ya Mgombea
urais wa Zanzibar DK. Hussein Ali Mwinyi ya kuipeleka Zanzibar katika maendeleo.
“Tunataka Zanzibar mpya ambayo imefanyiwa mageuzi, nimekwambia tunabadilisha awamu na tunakwenda awamu mpya hivyo tunataka Zanzibar mpya chini ya ndugu yetu Hussein Ali Mwinyi,” alisema
Akizungumzia eneo jengine la ratiba za mkutano huo wa kampeni alisema, wagombea hao watapata nasi ya kuzungumzia yale ambayo Chama cha Mpainduzi kinaenda kuyafanya kwa kipidi cha miaka mitano ijayo.
Katika maelezo yake alisema mgombea urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi
Polepole alisema, Dk. Mwinyi ndio mtu pekee mwenye uhalali wa kuisaidia
Zanzibar kukimbia haraka.
“Kama ambavyo ukiwasikiliza wazanzibari wanasema tunataka mtu fulani kama
alivyo Magufuli, ili yale ambayo yanafanyika Bara basi yafanyike hapa,
sasa huyo mtu wa kufanya kama Magufuli ni Hussein Ali Mwinyi,” alisema.
Alisema Dk.Mwinyi ndio mtu pekee mwenye uhalali wa kuisaidia Zanzibar
kukimbia haraka na kuviletea maendeleo visiwa vya Unguja na Pemba.
“Hapa Zanzibar tulitafuta sana ili tupate mtu muaminifu na muadilifu ambaye
anaweza kutusaidia kupata mabadiliko makubwa kwa maslahi ya Waanzibar ya kwenda mbele kwa kishindo ndipo tulipompata muungwana mmoja anayeitwa Hussein Ali Mwinyi,” alisema.
Alisema, Dk. Mwinyi ni kiongozi muandamizi ambaye amehudumu zaidi ya miaka 20 kwenye baraza la mawaziri ambapo ameongoza wizara nyeti ya ulinzi ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Polepole alisema, Dk. Mwinyi ni mtu mpole lakini ni makini na ni mkali kwa mambo ya ovyo na ni mtu muadilifu aisyekuwa na punje ya chembe ya kashfa na sio mropokaji.
“Dk. Mwinyi ni mtu ambaye ametulia na anaelewa kitu anachofanya halafu ni mtu anayefikika na hiyo ni sifa kubwa ya kiongozi,” alieleza
Katibu wa Uenezi Pole Pole alisema CCM haina upinzani visiwani Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kwamba itamshinda mgombea wa urais wa ACT-Wazalendo kwa kwa kishindo.
Alisema CCM kwa Zanzibar hakuna chama kinachoshindana nacho na iwe fundisho kwavyama vingine vya upinzani kuwa katika visiwani hapa hakuna mshindani wala upinzani na kwamba ni mtu mmoja amezungukwa na wanazi na anatumia upenyo huokupitia katiba na sheria kuendelea kubaki.
“Sasa watoto wadogo watamfundisha adabu ya kisiasa Seif Sharif Hamad kuwa
iwe ndio mwisho na kwamba hapa Zanzibar hakuna chama cha upinzani bali hapa
kuna mtu anateleza na katiba na sheria CCM itamshinda mgombea wa ACT-Wazalendomara tatu,”alisema
Akizungumzia maelekezo ya CCM alisema chama imetoa maelekezo kwa wagombea wake wa nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Zanzibar kujikita zaidi katika kunadi sera pamoja na muelekeo wa nchi endapo wakipata ridhaa ya kuiongoza serikali.
Katibu huyo alisema CCM kwa sasa wanajikita zaidi katika kuwaonyesha watanzania wapi nchi inapoelekea ila wapinzani wao wanadi sera za uongo pamoja na kujikita katika kupotosha watanzania.
Polepole alisema, CCM kwa hiari yake imeamua kutoa maagizo
kwa wagombea wao kujikita zaidi kutangaza muelekeo wa nchi wanapotaka
kuifikisha.
“Tumewaambia watangaze sera na muelekeo wa Taifa tunapotaka kulifikisha na si kutangaza tulichokifanya hapo nyuma maana watanzania tayari wameshayaona maendeleo makubwa yaliyofanywa na CCM,” alisema Polepole.
Aliongeza kuwa Wagombea wote wa nafasi ya urais kupitia CCM Rais Dk. John
Magufuli pamoja na Dk.Hussein Ali Mwinyi wajikite katika kutangaza maono ya
nchi wanapotaka kuifikisha pamoja na kutangaza maono yalikuwa katika Ilani ya
Chama ya mwaka 2020/2025.
“Mbali na kutangaza maono yao, wajikite zaidi katika kutangaza muelekeo wa
Ilani ya chama 2020/2025 huko kuna kila kitu ambacho kinaonesha wapi ambapo CCM inataka kuifanyia nchi hii,” alisema Polepole
Alisema tayari Rais Dk.Magufuli ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Dk.Mwinyi ambaye pia ni mgombea wa urais wa Zanzibarna viongozi wengine wakiwemo Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani wameshapita kutangaza muelekeo wa chama katika kuwafikisha watanzania.
Katibu Pole Pole alisema CCM inaendelea na kampeni zake kama ratiba zilivyopangwa ambapo hadi sasa tayari makundi mbalimbali yameshafikia kwa lengo la kunadi sera zao.
“Kwa upande wa Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wagombea wetu wameshawafikia makundi hayo na wanaendelea na Kampeni zao,”alisema Polepole
Katibu Pole Pole alisema mara nyingi visiwani hapa kumetokea vitendo vya
uvunjifu wa amani na akamatwi mtu na kwamba kuna siku walimwagiwa tindi kali mashekhe waliuwawa mapadri kutoka kanisa katoliki hakukamatwa mtu.
“Sasa msilete mambo hayo hii ni zama ya Amiri Jeshi Mkuu wa Rais Dk.Magufuli unapiga watu mapanga umeonekana unakamatwa unapelekwa kwenye vyombo vya sheria ninatoa maelekezo kama kiongozi wa CCM kwa jeshi la polisi kuhakikisha wanafanya upelelezi na wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,”alisema
Post a Comment