Featured

    Featured Posts

RC ANDENGENYE AMJULIA HALI ZITTO KABWE HOSPITALI

 


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amemtembelea na kutoa pole kwa Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma baada ya kupata ajali ya gari hapo jana wakati akiwa katika shughuli zake za kampeni.

Zitto Kabwe amepata ajali katika kata ya Kalya baada ya gari alilokuwa amepanda kugongwa na gari lingine kwa nyuma na kusababisha majeruhi kwa Watu waliokuwa katika gari hilo ambapo huduma ya kwanza walipatiwa katika Kituo cha Afya Kalya.

Zitto amesema gari lililowagonga na kusababisha ajali yao ni la Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa Ticket ya ACT, chanzo kikiwa ni vumbi lililokuwa limetanda Barabarani, ambapo amesema hali yake inaendelea kuimarika.

Kwa sasa tayari Zitto na Majeruhi wengine wamehamishiwa Dar Es Salaam kwa matibabu zaidi, mbali na Zitto, majeruhi wengine ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Said Rashid Bakema, Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Soily Simon Matete na Boaz Chuma (Mwanachama).

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana