Mkufunzi wa Inter Milan Antonio Conte ana mpango wa kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, ambaye kandarasi yake inatarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Calciomercato)
Ombi la West Ham la kumnunua mshambuliaji wa Norway Joshua King 28 lilikataliwa na Bournemouth. (Mail)
The Hammers bado wanaendelea na mazungumzo kuhusu usajili wa winga wa Brentford na Algeria Said Benrahma, 25. (Evening Standard)
West Ham wanakaribia kukubaliana dau la uhamisho la £25m kumsajili Benrahma kwa kutoa pamoja na marupurupu. (Guardian)
Everton pia ina hamu ya kumsajili mchezaji huyo. (Talksport)
Aliyekuwa winga wa Manchester United Memphis Depay hajapuuza uhamisho wa kuelekea Barcelona mwezi Januari . Mshambuliaji huyo wa Uholanzi alisalia na klabu ya Lyon ili kumaliza mwaka wake wa mwisho baada ya klabu hiyo ya Catalan kuwasilisha ombi msimu uliopita na klabu hiyo ya Ufaransa huenda ikamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la uhamisho la msimu ujao.. (Marca)
Mchezaji mpya wa United na Uruguay Facundo Pellistri, mwenye umri wa miaka 18 tayari anapanga kurudi nyumbani kwao kuichezea klabu ya Penarol klabu alioondoka ili kuhamia United.. (Sun)
Manchester City iliamua kumzuia beki wa Uhispania Eric Garcia kwa msimu mmoja kwasababu alikuwa na thamani kubwa kwao zaidi ya ofa ya Barcelona ya £18m , kulingana na ofisa wa operesheni Omar Berrada. Garcia, 19, anaweza kuhamia Nou Camp kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao baada ya kukataa kandarasi. (Manchester Evening News)
Mkufunzi wa Barcelona Ronald Koeman anasema kwamba mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 33, angesalia katika uwanja huo ili ili kuthibitisha umuhimu wake badala ya kuhamia Atletico Madrid.(Goal)
Post a Comment