Wananchi wa Jimbo la Ilemela wameombwa kumchagua kwa kipindi kingine aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa awamu iliyoisha ya mwaka 2015-2020 Mhe Dkt Angeline Mabula (pichani) kwa kuwa ndie aliyeshirikiana na Mhe Rais John Magufuli kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya Jimbo hilo na anaejua mipango ya maendeleo kwa awamu inayokuja.
Rai hiyo imetolewa na katibu wa Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha mapinduzi mkoa wa Mwanza (UWT) Bi Marry Muhoha wakati akihutubia wananchi wa kata ya Kahama katika viwanja vya shule ya msingi Kahama ikiwa ni muendelezo wa kampeni za mgombea ubunge kupitia CCM kwa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula ambapo amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumpa kura nyingi za ndio mgombea huyo itakapofika siku ya Oktoba 28, ili aweze kutangazwa mshindi na kuendeleza mazuri aliyoyaanzisha kwa kushirikiana na mgombea wa nafasi ya urais Mhe Dkt John Magufuli na diwani anaetokana na Chama hicho
'.. Dkt Mabula anafahamu changamoto za wana Kahama, anajua ametatua mpaka wapi?, Anajua bado wapi?, Tumchague yeye, tumchague Dkt Magufuli na diwani wakamalizie walipoishia, Yeye ndio mwenye ramani ya maendeleo yetu watu wa Kahama ..' Alisema
Kwa upande wake mgombea huyo wa Ubunge Dkt Angeline Mabula akasema kuwa kiasi Cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwaajili ya kuhakikisha kero ya kukosekana kwa umeme inakwenda kuisha ambapo umeme utafika katika maeneo yote ya Jimbo hilo sanjari na kuongeza kuwa kabla ya kipindi chake Cha awamu ya kwanza umeme ulikuwa ukipatikana kwa asilimia 35 na mpaka sasa umefikia asilimia 75 hivyo kuwaomba kumchagua tena ili akamalizie palipobakia.
.
Sambamba na kufafanua kuwa idadi ya vifo vya watoto wachanga imepungua kufikia vifo 3 Kati ya 1000 tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya kuboresha sekta ya afya ambapo zahanati mpya zaidi ya tano zimejengwa katika Jimbo hilo, hospitali ya wilaya imejengwa na kuboresha vituo vya afya vya Buzuruga, Sangabuye na Karume.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akawataka wananchi hao kutojaribu kuchagua wagombea wa vyama pinzani kwani kufanya hivyo ni kujicheleweshea maendeleo wakati meneja kampeni Ndugu Kazungu Safari Idebe akafafanua juu ya miradi iliyotekelezwa kwa kipindi Cha miaka 5 ya Mhe Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa shule mpya tatu nane, tatu msingi, tatu sekondari na mbili za kidato Cha tano na sita.
Post a Comment