Sehemu ya akina mama wakiwa katika kikao cha ndani cha kampeni za CCM za nyumbani kwa Mgombea Udiwani Kata ya Msalato, Dodoma,Nsubi Bukuku.
Katibu wa UWT Kata ya Msalato, Grace Chifungo akitoa maneno ya utangulizi wakati wa kikao hicho cha ndani cha kampeni.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Msalato, Jemina Nchimbi akimwaga sera nzuri za CCM, hivyo kuwataka wanawake wanawapigia kura wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa akielezea mikakati mbalimbali mbele ya wanawake wakiwemo na mabalozi wa mashina ya ushindi ambapo pia alielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ambaye ndiye Mgombea Urais wa Tganzania kupitia CCM.
Aliyekuwa mmoja wa wagombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia UWT, Sella Mkisi akijitambulisha wakati wa kikao hicho na kuwaomba wanawake kura zote kuwapigia wagombea wa CCM. Sella ni mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Wilaya ya Dodoma Mjini.
Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Msalato, Nsubi Bukuku wakati wa kikao hicho cha ndani.
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Wilaya ya Dodoma Mjini, Flora Liacho (katikati), akielezea jinsi anafahamu uchapakazi wa Mgombea Udiwani Kata ya Msalato, Nsubi Bukuku hivyo kuwaomba wanawake wanampigia kura ili ashirikiane nao kuwaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msalato, Lucia Mubao akiwasisitiza wanawake kuhakikisha Oktoba 28, mwaka huu wanampatia kura zote mgombea wao Nsubi Bukuku.
Aliyekuwa miongoni mwa wagombea ubunge Dodoma Mjini, Romana Nyoni akiwa amepiga magoti kuwaomba mabalozi na wananwake kwa ujumla kuhakikisha Oktoba 28, wanawapigia wagombea wa CCM akiwemo Nsubi.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Msalato kupitia CCM, Nsubi Bukuku (kulia), akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya Dodoma, ambaye yupo kwenye Kamati ya Ushindi, Romana Nyoni aliyepiga magoti akimuombea kura kwa akina mama pamoja na kumsihi akishinda uchaguzi awe mnyenyekevu kwa kuwatumikia vyema wananchi. Kikao hicho cha ndani kiliandaliwa na Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Dodoma.
Mgombea Udiwani Kata ya Msalato kupitia CCM, Nsubi Bukuku. (katikati), akicheza muziki na wanawake baada ya kikao cha ndani cha kampeni za CCM kumalizika nyumbani kwake Msalato, Dodoma.
Mmmoja wa akina mama akisikiliza kwa makini wakati Nsubi akiwaomba kura.Mke wa Mgombea Udiwani, Nsubi Bukuku, Joyce akimuombea kura mumewe na kuahidi kwamba akishinda wataanzisha Saccos ya kuwapesha wanawake katika kata hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Wilaya ya Dodoma Mjini, Joyce Smacus akiwaombea kura wagombea wa CCM, Dk. Magufuli, Anthony Mavunde na Nsubi Bukuku.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
Post a Comment