Club ya Yanga SC leo imeendelea kujiweka fiti kuelekea muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara itakayoendelea mara baada ya mechi za Kalenda ya FIFA kumalizika.
Yanga imecheza leo mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Licha ya Yanga kukosa kocha mkuu kwa sasa na baadhi ya wachezaji kwenda timu ya taifa, wameendelea kujifua chini ya kocha wao msaidizi Juma Mwambusi na mshambuliaji wao nyota Michael Sarpong ndio akafunga goli hilo dakika ya 81.
Post a Comment