Mitandao ya habari nchini Argentina imeripoti kuwa legend wa soka wa Argentina Diego Maradona (60) amefariki dunia wiki 2 baada ya kuruhusiwa hospitali.
Maradona inaripotiwa amefariki kwa tatizo la moyo (cardiac arrest), Maradona alipata tatizo la shambulio la moyo wiki mbili baada ya kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amefanyia upasuaji wa Ubongo.
Diego Maradona alifanyiwa upasuaji huo ili kuondoa tone la damu lililokuwa limeganda katika Ubongo, Maradona atakumbukwa kwa mchango na uwezo wake mkubwa uliyoisaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia 1986.
Post a Comment