Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inatoa taarifa rasmi kwa Wateja wake na kwa Umma kwa jumla kuwa, Ofisi ya Mkoa wa kihuduma ya DAWASA Tabata iliyokuwa Tabata Shule, sasa imehamia eneo la Tabata Segerea Chama. Hivyo kuanzia tarehe 16.11.2020, huduma zote zitatolewa katika ofisi hiyo mpya. Kwa maelezo zaidi, Tafadhali wasiliana nasi kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa namba ya kupiga bila malipo namba 0800110064 au 0736 451867 ya huduma kwa wateja DAWASA Tabata. #Dawasa tunawafikia
Jengo la Ofisi mpya ya DAWASA iliyopoTabata Segerea Chama.
Post a Comment