…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuwapokea wageni wote wanaotarajiwa kufika katika hafla ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule Dk John Magufuli zilizopangwa kufanyika Novemba 5,2020 kwenye uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.
Pia Kamanda Muroto ametoa onyo kali kwa watu watakaoandamana kuingia barabarani bila kufuata taratibu.
“Kwa ujumla jiji la Dodoma lipo salama kabisa kila mmoja anafanya shughuli zake za maendeleo,napenda kuwaambia wageni wote wanaotarajia kuja katika hafla za kuapishwa kwa Rais Mteule waje wakiwa na amani jeshi la polisi lipo na limeweka ulinzi katika kila kona ya eneo,”amesema Muroto.
Muroto amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kila kona kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jijini hapa.
Hata hivyo amesema kuwa kitu kinachoitwa maandamano haramu hakitakiwi barabarani, mtu akiingia barabarani inamaana anataka kulichokoza Jeshi la Polisi kutokana na kuwa kamanda Simon Sirro alishaeleza kuwa maandamano hayo ni haramu.
“Wale wamepigwa kwa kipigo cha mbwa kachoka kupitia kura za wananchi,Jeshi la Polisi litawapiga kwa kipigo cha mbwa koko kwa wale watakaojitokeza kufanya maandamano haramu,”amesema Muroto.
Post a Comment