Wanajeshi katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray wamefyatua maroketi katika jimbo jirani, katika mzozo wao na serikali ya Ethiopia unaoendelea kupanuka.
Hali ya uhasama baina ya seikali na wanajeshi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF), wanaodhibiti jimbo la Tigray, ilitokota na kusababisha makabiliano ya kijeshi mwezi huu.
Maafisa wamesema "maeneo ya viwanja vya ndege " yameharibiwa katika shambulio la maroketi. TPLF walithibitisha kuhusika, wakisema kuwa mashambulio yalikuwa ni ya ulipizaji kisasi.
Mashambulio haya yametokea baada ya mauaji
Shirika la ya kutetea haki za biandamu la Amnesty International limesema limethibitisha kwamba "Wengi , na huenda mamia ya watu, walichomwa visu au kukatwakatwa hadi kufa " katika mji wa Mai-Kadra (May Cadera) tarehe 9 Novemba.
Waziri mkuu Minister Abiy Ahmed amewashutumu vikosi vinavyowatii viongozi wa Tigray kwa kufanya mauaji ya watu wengi, lakini TPLF wamekanusha kuhusika.
Bw Abiy aliamuru kufanyika kwa harakati za kijeshi dhidi ya TPLF mapema mwezi huu baada ya kuwashutumu kushambulia kambi ya kijeshi ya wanajeshi wa shirikisho - madai yanayokanushwa na TPLF. Kumekuwa na makabiliano kadhaa na mashambulio ya anga katika jimbo hilo.
Mapigano hayo mabaya yamewalazimisha maelfu ya raia kuvuka mpaka na kuingia Sudan, ambayo inasema itawapatia hifadhi katika kambi ya wakimbizi.
Kupata taarifa zilizo huru kuhusu hali ya mambo katika jimbo la Tigray ni vigumu kwasababu laini za simu na huduma ya mtandao havipatikani kwa urahisi.
Tunachokifahamu kuhusu shambulio la roketi?
Kikosi kazi cha dharura cha serikali ya Ethiopia kilisema maroketi yalifyatuliwa kuelekea katika miji ya Bahir Dar na Gondar, katika jimbo la Amhara, Ijumaa jioni.
" TPLF junta inatumia silaha za mwisho zilizosalia kwenye akaba yake," iliandika katika taarifa, na kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa.
Afisa ameliambia Shirika la habari la Reuters kwamba roketi moja ilipiga uwanja wa ndege uliopo Gondar na kuuharibu kidogo, huku yapili ilianguka tu nje ya uwanja wa ndege wa Bahir Dar.
Taarifa kuhusu majeruhi hazitolewa mara moja wazi.
Viwanja vyote vya ndege hutumiwa na ndege za kijeshi pamoja na za raia.
Vikosi kutoka Amhara vimekuwa vikipigana sambamba na vikosi vya serikali kuu ya shirikisho dhidi ya wapiganaji wa Tigray.
TPLF imesema kuwa shambulio la roketi lilikuwa ni la kulipiza kisasi kwa shambulio la hivi karibuni lililofanywa na vikosi vya Bw Abiy.
"Kama mashambulio dhidi ya watu wa Tigray hayatasitishwa, mashambulio yataimarika ," alisema msemaji.
Shambulio la roketi limeibua hali uya wasiwasi kwamba mapigano katika jimbo la Ethiopia lililoko kaskazini zaidi yanaweza kusambaa katika maeneo mengine ya nchi.
Kulikuwa na mauaji ya watu wengi katika Tigray?
Shirika la AmnestyInternational linasema kuwa ushahidi unaonesha watu " kadhaa" waliuawa na kujeruhiwa kwa kisu au panga katika mashambulio ya Mai-Kadra
Lilisema kuwa liliona na kushuhudia " picha za kutisha zilizothibitishwa kidigitali pamoja na video za miili ya watu waliokuwa wametapakaa katika mji au wakichukuliwa katika machela ".
Amnesty linasema kuwa wahanga walionekana kuwa walikuwa ni wafanyakazi na hawakuhusika katika mzozo. Haifahamiki ni wapi walikotoka.
Tume ya haki za binadamu ya Ethiopia ilisema kuwa itatuma timu ya kufanya uchunguzi wa taarifa hizo.
Bw Mr Abiy amevishutumu vikosi vinavyowatii viongozi wa Tigray kwa kutekeleza mauaji hayo akisema vilifanya uvamizi baada ya wanajeshi wa muungano "kukomboa" eneo la magharibi mwa Tigray.
Baadhi ya walioshuhudia wanasema pia kuwa shambulio lilitekezwa na vikosi vinavyotii TPLF baada ya kushindwa na vikosi vya serikali kuu ya shirikisho katika eneo linaloitwa a Lugdi.
Kiongozi wa Tigray Debretsion Gebremichael aliliambia shirika la habari la AFP nkwamba shutuma hizo "hazina msingi ".
Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa mauaji hayo yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Ni kwanini serikali ya Ethiopia na TPLF wanapigana?
Hali ya wasi wasi imekuwa ikiongezeka kwa muda mrefu na uhusiano kati ya TPLF na serikali kuu umezota
TPLF ilitawala jeshi la Ethiopia na maisha ya kisiasa kwa miongo kadhaa kabla ya Bw Abiy kuingia mamlakani mwaka 2018 na kupitisha mageuzi mkubwa.
mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa ka misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja , national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.
Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.
Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki "usiokuwa na kanuni "
Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzoz wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.
Kwa upande wake, waziri mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanadharau mamlaka yake.
Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka "mstari wa mwisho mwekundu".
Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi
Post a Comment