MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA NA PROF KABUDI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI MJINI GABORONE, BOTSWANA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika leo Tarehe 27, Novemba 2020, mjini Gaborone Botswana. Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Utatu wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Msumbiji uliofanyika leo Tarehe 27, Novemba 2020, mjini Gaborone Botswana, (Picha zote na Nelson Kessy)
Post a Comment