Barcelona huenda ikamnyatia mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane, 28, au kiungo wa kati wa Uholanzi Gini Wijnaldum, 30, baada ya kipengee katika makubaliano yaliyowezesha Philippe Coutinho kwenda Nou Camp kumalizika - Barca kusajili mchezaji mwingine wa Liverpool italazimika kulipa kitita cha ziada cha pauni milioni 89. (Star)
Mgombea urais wa Barcelona Emili Rousaud anasema ikiwa atachaguliwa atasajili "wachezaji wawili wazuri, mmoja wao akiwa Neymar", mshambuliaji wa Brazil, 28, ambaye aliweka rekodi ya dunia ya uhamisho kutoka Barca hadi Paris St Germain mwaka 2017. (Marca - in Spanish)
Lyon imetupilia mbali hatua ya kumsaka mchezaji wa Arsenal Houssem Aouar kwasababu ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Reims ambapo kiungo huyo wa kati, 22, raia wa Ufarasa alikataa kupasha misuli moto kwasababu hakutumika kama mchezaji wa akiba kwenye mechi hiyo dhidi ya Angers walioibuka na ushindi. (L'Equipe via Mirror)
Manchester United bado haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele lakini itajitahidi kufikia makubaliano ya mkopo kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 23. (Sport - in Spanish)
Mkurugenzi wa Borussia Dortmund Michael Zorc anaona mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland ataendelea kusalia katika klabu hiyo "kwa muda mrefu" licha ya mchezaji huyo, 20, kuhusishwa na kuhamia Real Madrid. (Goal)
Chelsea inamnyatia beki wa kati wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25. (Sun)
Tottenham iko tayari kumsajili winga wa Leicester Demarai Gray, 24, kwa uhamisho wa bila malipo Januari. (Express)
Liverpool huenda ikapata kima cha pauni milioni 30 dirisha la usajili litakapofunguliwa Januari kwa kumuuza kiungo wa kati wa Uswisi Xherdan Shaqiri, 29, na mshambuiaji wa Ubelgiji Divock Origi, 25. (Express)
Mlinda lango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 21, anakaribia kukubali mkataba mpya na AC Milan. (Calciomercato - in Italian)
Manchester United imetoa ofa mpya kwa mchezaji Timothy Fosu-Mensah,22, wa Uholanzi anayeweza kucheza nafasi kadhaa ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. (Manchester Evening News)
West Brom inamfuatilia kiungo wa kati wa Celtic raia wa Ufaransa Ntcham, 24. (Football Insider)
Aston Villa huenda ikatenga kitita cha pesa Januari kwa ajili ya winga wa Werder Bremen raia wa Kosovo Milot Rashica, 24, ambaye pia amehusishwa na RB Leipzig, Bayer Leverkusen na Wolfsburg. (Kreiszeitung - in German)
Mchezaji wa QPR Bright Osayi-Samuel ameambiwa aache kuwa na wasiwasi huku winga huyo mzaliwa wa Nigeria, 22, akihusishwa na Burnley, Celtic, Fulham, Leeds United na Leicester. (LancsLive)
Ligi ya soka Uingereza haitabadilisha mechi zilizopangwa kuchezwa siku ya mwisho ya kutekelezwa kwa hatua ya kusalia ndani ili watu waweze kuhudhuria mechi hizo siku moja baadaye. (Mail)
Post a Comment