Featured

    Featured Posts

MBUNGE BAHATI NDINGO, 'AMWAGA' MISAADA YA VIFAA TIBA KATIKA WODI YA WAZAZI SINZA, VYAKULA NA MAHITAJI MENGINE KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA KIBAHA.

Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndingo akiwakabidhi watoto sehemu ya Msaada wa vyakula na mahitaji mbalimbali, alipotoa msaada wa vitu hivyo kwa Kituo cha Watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Buloma Foundation, kilichopo eneo la Sofu, Kibaha mjini mkoa wa Pwani, jana. Baadhi ya msaada huo aliotoa ni mchele, sukari, unga, dawa za kusukutulia meno, miswaki, biskuti na vinywaji visivyo la kilevi. Baadhi ya wengine kutoka kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Pwani Gama J. Gama, Mwenyekiti wa Jumiya hiyo mkoa wa Pwani Jackson Kituka, Diwani Mteule wa Viti Maalum Kibaha mjini Selina Wilsnon na anayesaidia na Mbunge huyo kuwapatia watoto sehemu ya msaada huo ni Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo hicho Anna Kyando.

Mwanzo👇

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, mkoa wa Pwani Gama J. Gama akimkaribisha Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndingo alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kabla ya kwenda kutoa msaada wake kwenye Kituo cha Watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Buloma Foundation, kilichopo eneo la Sofu, Kibaha mjini mkoa wa Pwani, jana. Baadhi ya msaada huo aliotoa ni mchele, Katikati ni Katibu wa Siasa Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia hiyoMohammed Cholaje.
 Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndingo akilakiwa na aliyekuwa mtia nia ya kuwania nafasi hiyo ya Ubunge kwa tiketi ya CCM kupitia Jumuiya hiyo Helena Madanja, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kabla ya kwenda kutoa msaada wake kwenye Kituo cha Watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Buloma Foundation, kilichopo eneo la Sofu, Kibaha mjini mkoa wa Pwani, jana. Baadhi ya msaada huo aliotoa ni mchele, Katikati ni Katibu wa Siasa Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia hiyoMohammed Cholaje.
Helena Madanja na Mbunge huyo wakisalimiana kwa bashasha.
 Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndingo akisaini kitabu cha wageni, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kabla ya kwenda kutoa msaada wake kwenye Kituo cha Watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Buloma Foundation, kilichopo eneo la Sofu, Kibaha mjini mkoa wa Pwani, jana.
 Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndingo akiendelea kusaini vitabu vya wageni. Kushoto ni Katibu wa Siasa Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia hiyoMohammed Cholaje pia akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Dk. Zainab Gama, na anayewashuhudia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa pwani Jackson Kituka.
Watumishi wa CCM mkoa wa Pwani Mary Nchimbi na mwenzake wakijadiliana jambo la kikazi, kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani Jackson Kituka akizungumza kukaribisha ugeni.
Cholaje na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani wakitoka nje baada ya mazungumzo. Kushoto ni Mbunge huyo na aliyekuwa mtia nia ya Ubunge wa viti maalum kupitia Jumiya hiyo Helena Madanja wakiendelea kufuahiana wakati wakitoka umbumbini.

Kuwasili Kituo cha Buloma Foundation👇

Diwani wa Kibaha Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mjini Mussa Ndomba na Diwani Mteule wa katika eneo hilo  Selina Wilson wakiongoza baadhi ya viongozi kwenda kupokea Ugeni.
Diwani Ndomba akitambulishwa kwa Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM kupitia Jumuia ya Wazi Tanzania Bahati Ndingo na  Mwenyekiti wa Jumjuiya hiyo mkoa wa Pwani, baada ya ugeni kuwasili.
Diwani mteule wa Viti Maalum Kibaha mjini Selina Wilson naye akitambulishwa kwa Mbunge huyo.
Watoto wa Kituo cha Buloma Foundation wakiwa tayari kumvisha skafu maalum ya Bendera ya Taifa Mbunge huyo (kulia), alipowasili
Mbunge huyo akiwa amechuchumaa ili kulingana kimo na watoto hao wakati wakimvalisha skafu hiyo.
Mbunge huyo (kulia) akishirikiana na watoto hao kuimba wimbo kuimba wimbo wa mapokezi waliokuwa wakimwuimbia kama sehemu ya kumkaribisha kituoni kwao

Diwani mteule wa Viti Maalum Kibaha mjini Selina Wilson akiwa amembeba kwa furaha mmoja wa watoto wa kituo hicho baada ya wageni kutekti
Mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Kyando akimpokea kwa furaha iliyochanganyika na majonzi Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania Bahati Ndingo alipowasili kwenye kituo hicho kutoa msaada wake. Kulia ni aliyekuwa mtia nia ya Ubunge kwa tiketi ya Jumuia hiyo Helena Mataja akimfariji Anna Kyando.

Mbunge Bahati akikabidhi misaada👇

Mbunge huyo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Kyando kuhusu msaada aliokuwa akikabidhi.
Mbunge Bahati akikabidhi msaada huo kwa baadhi ya watoto walioteuliwa kushiriki kuupokea huku wakisaidiwa na Mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Kyando.
"Haya watoto nimewaletea pia miswaki", akasema Mbunge Bahati wakati akiendelea kukabidhi misaada hiyo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani akifanya utambulisho.
Diwani Ndomba akisimama kupokea heshima ya kutambulishwa.
Diwani Mteule Selina Wilson akipunga mkono kupokea heshima ya kutambulishwa
Kisha Diwani huyo akasema, "CCM Hoyeeee, Watoto safiii...." huku akitabasamu.
Mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Kyando akisalimia na kusema machache baada ya kutambulishwa.
Cholaje akisitisha kwamanza mambo mengine ili watoto 'wajinafasi' kwa soda alizowapatia Mbunge Bahati.

Watoto wa wakipoza makoo yao kwa Soda hizo👇




Risala kwa Mbunge Bahati na msafara wake👇
"Meshimiwa Mbunge na Ujumbe wako, kwanza tunakushuru kwa kuja kututembelea na kutuletea zawadi kem kem...Pia tunayo mwengi ya kukueleza lakini kwa leo tunaomba kukueleza kuwa miongozi mwa changamoto tulizonazo kwenye kituo chetu ni uzio kwani eneo letu ni Square Meter 5230, na tumefanikiwa kupata waya wa uzio roller 32 ambazo tumechangiwa na wasamaria wema, kwa hiyo tunauhitaji wa vifaa vya kushikilia uzio kama ifuatavyo; Nguzo 140, Mifuko 26 ya Saruji, Lori mbili za kokoto, lori mbili za mchanga,  Kench Wire roller 2, Unails Kg 8, Gate Nondo 8, Rem Bem 24, Geti Kubwa na Senyenge ambavyo gharama zake vyote ikiwemo na ufundi ni sh. 3,475,400" akasema mtoto aliyesoma risala hiyo.
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge Bahati👇

Hotuba👇

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazzi mkoa wa Pwani akimkaribisha Mgnei rasmi kuzungumza.
"Mheshimiwa Mbunge, Hapa tupo vizuri, unavyotuna hapa viongozi wengi tunaishi katika eneo hili la Sofu..." akasema Mwenyekiti huyo.
"Na huyu Diwani wetu mteule Selina Wilson na Diwani wa Kibaha mjini huyu Ndoma (kulia) wote wanaishi hapa, na mimi pia naishi hapa", akasema Mwenyekiti huyo. Kisha akamkaribisha Mheshimiwa Mbunge kuongea na hadhara.
Meza Kuu wakasimama pamoja na Mbunge kumpa heshima
Mbunge wa viti malaum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Bahati Ndigo akizungumza mengi, lakini akasisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuwasaidia wenye uhitaji kama walivyo watoto kwenye Kituo hicho cha Buloma, Kisha akaahidi kushirikiana na kituo hicho katika kutoa msaada wa nguzo 140 zilizoombwa na kituo kupitia risala.
"Tunaposema Jumuiya hii ya Wazazi, moja ya makujumu yetu ni kuangalia jamii yetu, hasa watoto yatima na wanaoshi kwenye mazingira magumu na wazee na kina mama weneye uhitaji, kwa hiyo mimi kwa nafasi yangu hii ya Ubunge niliyoipata kupitia Jumuiya hii, nimeona ninao wajibu kuja kusaidia Kituo hiki" alisema Mbunge Bahati.

Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania Mohamed Cholaje akazungumza kufunga shughuli hiyo, lakini akasisitiza kwamba katika ujenzi wa uzio wa kituo hicho Jumuya ya Wazazi itabidi ibebe jukumu la kujitoea baadhi ya maeneo ikiwemo ufundi na kuchimba mashimo ya kupachika nguzo.

Watoto wakiimba wimbo wa kumuaga mgeni👇


Picha ya Pamoja Mbunge na watoto, watumishi wa kituo Kituo na baadhi ya Viongozi kuhitimisha hafla👇



Kuagana na kupongezana👇





"Haya kwa herini jamani, nitakuja simu nyingine panapo majaaliwa ya Mungu", akasema Mbunge wakati anaaga.


Msaada wa Vifaa tiba, Hospitali ya Sinza, jijini Dar es Salaam👇

Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania Bahati Ndingo akikabidhi vifaatiba kwa viongozi wa manispaa ya Ubungo wakati alipofika kutoa msaada wa vifaa hivyo kwa kina mama kwenye wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Sinza wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na wapili kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Leonard Peter Nsanya, 

Zinazofuata ni Picha mbalimbali kuhusiana na makabiano hayo👇








Mbunge Bahati na Ujumbe wake wakiwa Ofisi ya CCM Kata ya Sinza kukamilisha itikafaki👇






Ends
// Picha na Maelezo na Bashir Nkoromo, CCM Blog
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana