Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MLINDA mlango, Metacha Boniphace Mnata leo ameinusuru klabu yake, Yanga SC kupoteza mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuokoa mkwaju wa penalti wa dakika ya mwisho wa Mrundi, Bigirimana Blaise timu hiyo ikitoa sare ya 1-1 na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Mnata aliuchupia mkwaju huo na kuupangua kabla ya kuuondosha hatarini na kuamsha shangwe za mashabiki wa timu ya Jangwani – wakishukuru kwa sare ya nyumbani kuliko kupoteza mechi.
Post a Comment